1 Chronicles 19:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waamoni walipoona wamejifanya wachukizwe na Daudi, Hanuni na hao Waamoni walituma watu wapeleke talanta 4,000 za fedha kukodisha magari na wapandafarasi kutoka Mesopotamia, Aramaaka na Soba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waamoni walipotambua kwamba wamekuwa machukizo kwa Daudi, basi Hanuni na Waamoni wakatuma talanta elfu moja za fedha ili kukodisha magari ya vita, pamoja na waendeshaji wa hayo magari ya kukokotwa na farasi, kutoka Mesopotamia, Aram-Maaka na Soba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wana wa Amoni walipoona ya kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Hanuni na wana wa Amoni wakapeleka talanta elfu za fedha ili kujiajiria magari na wapanda farasi kutoka Mesopotamia, na kutoka Atam-maaka, na kutoka Soba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waamoni walipoona wamejifanya wachukizwe na Daudi, Hanuni na hao Waamoni walituma watu wapeleke talanta 4,000 za fedha kukodisha magari na wapandafarasi kutoka Mesopotamia, Aramaaka na Soba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waamoni walipogundua kwamba wamekuwa harufu mbaya puani mwa Daudi, Hanuni na Waamoni wakatuma talanta 1,000 za fedha ili kukodisha magari ya vita pamoja na waendeshaji wa hayo magari ya kukokotwa na farasi, kutoka Aramu-Naharaimu, Aramu-Maaka na Soba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Hanuni na Waamoni wakatuma talanta 1,000 za fedha ili kukodisha magari ya vita pamoja na waendeshaji wa hayo magari ya kukokotwa na farasi, kutoka Aramu-Naharaimu, Aramu-Maaka na Soba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wana wa Amoni walipoona ya kuwa wamejisababishia machukizo kwa Daudi, Hanuni na wana wa Amoni wakatuma talanta elfu moja za fedha ili kukodi magari na wapanda farasi kutoka Mesopotamia, na kutoka Atam-maaka, na kutoka Soba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waamoni walipoona wamejifanya wachukizwe na Daudi, Hanuni na hao Waamoni walituma watu wapeleke talanta 4,000 za fedha kukodisha magari na wapandafarasi kutoka Mesopotamia, Aramaaka na Soba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Amoni walipoona, ya kuwa wamejichukizisha kwake Dawidi, ndipo, Hanuni na wana wa Amoni walipotuma vipande elfu vya fedha, ndio shilingi milioni moja na 200000, wakodishe magari na wapanda farasi kwa Washami wa Mesopotamia na kwa Washami wa Maka nako Soba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wana wa Amoni walipoona ya kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Hanuni na wana wa Amoni wakapeleka talanta elfu za fedha ili kujiajiria magari na wapanda farasi kutoka Mesopotamia, na kutoka Atam-maaka, na kutoka Soba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waamoni walipoona wamejifanya wachukizwe na Daudi, Hanuni na wale Waamoni wakatuma watu wapeleke kilo elfu makumi tatu za feza kwa kulipa magari ya vita na waaskari wapanda-farasi kutoka Mesopotamia, Aramaka na Zoba.