1 Chronicles 19:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walikodisha magari 32,000 na mfalme wa Maaka na askari wake, akaja na kupiga kambi karibu na Medeba. Waamoni walikusanyika toka kwenye miji yao yote, wakajiandaa tayari kwa vita.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakakodisha magari ya vita elfu thelathini na mbili na waendeshaji wake, pamoja na mfalme wa Maaka na vikosi vyake. Wakapiga kambi karibu na Medeba. Waamoni nao wakakusanyika toka miji yao, wakatoka ili kupigana vita.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakajiajiria magari thelathini na mbili elfu, na mfalme wa Maaka na watu wake; nao walikuja wakatua mbele ya Medeba. Na wana wa Amoni wakakusanyika kutoka miji yao, wakaja vitani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walikodisha magari 32,000 na mfalme wa Maaka na askari wake, akaja na kupiga kambi karibu na Medeba. Waamoni walikusanyika toka kwenye miji yao yote, wakajiandaa tayari kwa vita.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakakodisha magari ya vita 32,000 yakiwa na waendeshaji wake, pamoja na mfalme wa Maaka na vikosi vyake, wakaja na kupiga kambi karibu na Medeba. Waamoni nao wakakusanyika toka miji yao, wakatoka ili kupigana vita.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakakodisha magari ya vita 32,000 yakiwa na waendeshaji wake, pamoja na mfalme wa Maaka na vikosi vyake, wakaja na kupiga kambi karibu na Medeba. Waamoni nao wakakusanyika toka miji yao, wakatoka ili kupigana vita.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakakodi magari elfu thelathini na mbili, na mfalme wa Maaka na watu wake; nao walikuja wakatua mbele ya Medeba. Na wana wa Amoni wakakusanyika kutoka miji yao, wakaja vitani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walikodisha magari 32,000 na mfalme wa Maaka na askari wake, akaja na kupiga kambi karibu na Medeba. Waamoni walikusanyika toka kwenye miji yao yote, wakajiandaa tayari kwa vita.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakakodisha magari 32000 pamoja na mfalme wa Maka na watu wake, wakaja, wakapiga makambi mbele ya Medeba, nao wana wa Amoni wakakusanyika wakitoka mijini kwao, wakaja vitani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakajiajiria magari thelathini na mbili elfu, na mfalme wa Maaka na watu wake; nao walikuja wakatua mbele ya Medeba. Na wana wa Amoni wakakusanyika kutoka miji yao, wakaja vitani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walikopesha magari elfu makumi tatu na mawili, na mufalme wa Maka na waaskari wake akakuja na kupiga kambi karibu na Medeba. Waamoni walikusanyika toka kwenye miji yao yote, wakajiweka tayari kwa vita.