1 Chronicles 19:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waamoni walitoka wakajipanga kwenye lango la mji, hali wale wafalme waliokuja walikuwa peke yao kwenye tambarare.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waamoni wakatoka, wakajipanga wakiwa tayari kwa vita langoni la mji wao, wakati wale wafalme wengine waliokuja nao walijipanga kwa vita uwanjani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakatoka wana wa Amoni, wakapanga vita langoni pa mji; na hao wafalme waliokuja walikuwa peke yao uwandani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waamoni walitoka wakajipanga kwenye lango la mji, hali wale wafalme waliokuja walikuwa peke yao kwenye tambarare.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waamoni wakatoka wakajipanga tayari kwa vita katika ingilio la mji wao, wakati ambapo wale wafalme wengine waliokuja nao walijipanga kwa vita uwanjani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waamoni wakatoka wakajipanga wakiwa tayari kwa vita langoni la mji wao, wakati wale wafalme wengine waliokuja nao walijipanga kwa vita uwanjani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakatoka wana wa Amoni, wakajipanga kwa vita langoni pa mji; na hao wafalme waliokuja walikuwa peke yao uwanjani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waamoni walitoka wakajipanga kwenye lango la mji, hali wale wafalme waliokuja walikuwa peke yao kwenye tambarare.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Amoni wakatoka, wakajipanga penye lango la mji, wapige vita, nao wafalme waliokuja wakawa peke yao shambani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakatoka wana wa Amoni, wakapanga vita langoni pa mji; na hao wafalme waliokuja walikuwa peke yao uwandani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waamoni wakatoka na kujipanga kwenye mulango wa muji, wakati wale wafalme waliokuja walikuwa peke yao kwenye mbuga.