1 Chronicles 20:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata ikawa katika mwanzo wa mwaka mpya, wakati ambapo wafalme huenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi na kuteka nyara nchi ya Waamoni, pia akaenda na kuuzingira Raba. Lakini Daudi alibaki huko Yerusalemu. Naye Yoabu aliushambulia Raba na kuuharibu;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwanzoni mwa mwaka mpya, wakati wafalme huenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi. Aliangamiza nchi ya Waamoni, na akaenda Raba na kuuzingira, lakini Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu akashambulia Raba na kuuacha ukiwa magofu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Yoabu akawaongoza mashujaa wa jeshi, akaiteka nyara nchi ya wana wa Amoni, akaja akauhusuru Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu. Naye Yoabu akaupiga Raba akauangamiza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata ikawa katika mwanzo wa mwaka mpya, wakati ambapo wafalme huenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi na kuteka nyara nchi ya Waamoni, pia akaenda na kuuzingira Raba. Lakini Daudi alibaki huko Yerusalemu. Naye Yoabu aliushambulia Raba na kuuharibu;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwanzoni mwa mwaka mpya, wakati ambapo wafalme hutoka kwenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi. Aliangamiza nchi ya Waamoni akaenda Raba na kuuzunguka huo mji kwa Jeshi, lakini Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu akaushambulia Raba na kuuacha ukiwa magofu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwanzoni mwa mwaka mpya, wakati ambapo wafalme huenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi. Aliangamiza nchi ya Waamoni, na akaenda Raba na kuuzingira, lakini Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu akashambulia Raba na kuuacha ukiwa magofu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Yoabu akawaongoza mashujaa wa jeshi, akaiteka nyara nchi ya wana wa Amoni, akaja akauzingira Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu. Naye Yoabu akaupiga Raba akauangamiza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata ikawa katika mwanzo wa mwaka mpya, wakati ambapo wafalme huenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi na kuteka nyara nchi ya Waamoni, pia akaenda na kuuzingira Raba. Lakini Daudi alibaki huko Yerusalemu. Naye Yoabu aliushambulia Raba na kuuharibu;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, mwaka ulipopita, siku hizo, wafalme wanapozoea kwenda vitani, Yoabu akavipeleka vikosi vya askari, akaiangamiza nchi ya wana wa Amoni, akaja, akausonga mji wa Raba kwa kuuzinga, lakini Dawidi alikuwa anakaa Yerusalemu. Yoabu akaupiga Raba, akaubomoa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Yoabu akawaongoza mashujaa wa jeshi, akaiteka nyara nchi ya wana wa Amoni, akaja akauhusuru Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu. Naye Yoabu akaupiga Raba akauangamiza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ilipokuwa wakati wa kipwa, wakati ambapo wafalme wanaenda kwa vita, Yoabu akaongoza jeshi na kuharibu inchi ya Waamoni, akaenda vilevile na kuzunguka muji wa Raba kwa vita. Lakini Daudi alibaki kule Yerusalema. Naye Yoabu akashambulia muji wa Raba na kuuteka.