1 Chronicles 20:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
naye Daudi akaichukua taji ya mungu wao Milkomu kichwani pake; naye aligundua ya kwamba taji hiyo ilikuwa na uzito wa kilo thelathini na tano za dhahabu na ndani yake mlikuwemo kito cha thamani. Naye Daudi akakitwaa kupambia taji yake. Pia, aliteka idadi kubwa ya nyara kutoka katika mji huo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akachukua taji kutoka kwa kichwa cha mfalme wao, lililokuwa na uzito wa talanta moja ya dhahabu, nalo lilizungushiwa vito vya thamani. Likawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Alichukua nyara nyingi kutoka mji huo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Daudi akamtwalia mfalme wao taji toka kichwani pake, akaona ya kwamba uzani wake ni talanta ya dhahabu, na kulikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani; akazitoa nyara za mji, nyingi sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
naye Daudi akaichukua taji ya mungu wao Milkomu kichwani pake; naye aligundua ya kwamba taji hiyo ilikuwa na uzito wa kilo thelathini na tano za dhahabu na ndani yake mlikuwemo kito cha thamani. Naye Daudi akakitwaa kupambia taji yake. Pia, aliteka idadi kubwa ya nyara kutoka katika mji huo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akachukua taji kutoka kwenye kichwa cha mfalme wao, uzito wake ulikuwa talanta moja ya dhahabu na ilizungushiwa vito vya thamani. Ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Alichukua kiasi kikubwa cha nyara kutoka katika mji huo
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akachukua taji kutoka kwa kichwa cha mfalme wao, lililokuwa na uzito wa talanta moja ya dhahabu, nayo ilizungushiwa vito vya thamani. Ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Alichukua nyara nyingi kutoka mjini huo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Daudi akatwaa taji la Milkomu toka kichwani pake, akaona ya kwamba uzani wake ni talanta ya dhahabu, na kulikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani; akazitoa nyara za mji, nyingi sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
naye Daudi akaichukua taji ya mungu wao Milkomu kichwani pake; naye aligundua ya kwamba taji hiyo ilikuwa na uzito wa kilo thelathini na tano za dhahabu na ndani yake mlikuwemo kito cha thamani. Naye Daudi akakitwaa kupambia taji yake. Pia, aliteka idadi kubwa ya nyara kutoka katika mji huo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Dawidi alipoliondoa taji la mfalme wao kichwani pake, akaliona uzito wake kuwa frasila tatu za dhahabu, nalo lilikuwa limepambwa kwa vito vyenye kima; hilo Dawidi akavikwa kichwani. Namo mjini akatoa mateka mengi sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Daudi akamtwalia mfalme wao taji toka kichwani pake, akaona ya kwamba uzani wake ni talanta ya dhahabu, na kulikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani; akazitoa nyara za mji, nyingi sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Daudi akatwaa taji ya mufalme wao kutoka juu ya kichwa chake, naye akagundua kwamba taji hiyo ilikuwa na uzito wa kilo makumi tatu na tano za zahabu na ndani yake mulikuwa jiwe la bei kali. Daudi akavikwa taji hiyo juu ya kichwa chake. Vilevile alinyanganya vitu vingi sana kutoka katika muji ule.