1 Chronicles 20:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu aliwachukua watu wa mji huo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sururu za chuma na mashoka ya chuma. Hivyo ndivyo alivyoitenda miji yote ya Waamoni. Hatimaye Daudi na watu wote wakarudi Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawatoa watu waliokuwa humo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sululu za chuma na mashoka. Daudi akafanya hivi kwa miji yote ya Waamoni. Kisha Daudi na jeshi lake lote wakarudi Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hao watu waliokuwamo akawatoa, akawakata-kata kwa misumeno, na kwa sululu za chuma, na kwa mashoka. Ndivyo alivyofanya Daudi kwa miji yote ya wana wa Amoni. Nao wakarudi Yerusalemu Daudi na watu wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu aliwachukua watu wa mji huo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sururu za chuma na mashoka ya chuma. Hivyo ndivyo alivyoitenda miji yote ya Waamoni. Hatimaye Daudi na watu wote wakarudi Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na akawatoa watu waliokuwa humo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sululu za chuma na mashoka. Daudi akafanya hivi kwa miji yote ya Waamoni. Kisha Daudi na jeshi lake lote wakarudi Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawatoa watu waliokuwa humo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sululu za chuma na mashoka. Daudi akafanya hivi kwa miji yote ya Waamoni. Kisha Daudi na jeshi lake lote wakarudi Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hao watu waliokuwamo akawatoa, akawafanyisha kazi kwa misumeno, na kwa sululu za chuma, na kwa mashoka. Ndivyo alivyofanya Daudi kwa miji yote ya wana wa Amoni. Nao wakarudi Yerusalemu Daudi na watu wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu aliwachukua watu wa mji huo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sururu za chuma na mashoka ya chuma. Hivyo ndivyo alivyoitenda miji yote ya Waamoni. Hatimaye Daudi na watu wote wakarudi Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watu waliokuwamo akawatoa, akawakatakata kwa misumeno na kwa magari ya chuma ya kupuria na kwa mashoka. Hivyo Dawidi akaifanyizia miji yote ya wana wa Amoni. Kisha Dawidi akarudi Yerusalemu pamoja na watu wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hao watu waliokuwamo akawatoa, akawakata-kata kwa misumeno, na kwa sululu za chuma, na kwa mashoka. Ndivyo alivyofanya Daudi kwa miji yote ya wana wa Amoni. Nao wakarudi Yerusalemu Daudi na watu wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu akakamata watu wa muji ule, nao wakafanya kazi wakitumia misumeno, sururu za chuma na mashoka ya chuma. Ni vile ndivyo alivyoitendea miji yote ya Waamoni. Kisha Daudi na watu wote wakarudi Yerusalema.