1 Chronicles 20:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulitokea tena vita na Wafilisti. Naye Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mpini wa mkuki wake, ulikuwa kama mti wa mfumaji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kulikuwa na vita tena na Wafilisti; na Elhanani, mwana wa Yairi akamwua Lahmi nduguye Goliathi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulitokea tena vita na Wafilisti. Naye Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mpini wa mkuki wake, ulikuwa kama mti wa mfumaji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimwua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mpini wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kulikuwa na vita tena na Wafilisti; na Elhanani, mwana wa Yairi akamwua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mti wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulitokea tena vita na Wafilisti. Naye Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mpini wa mkuki wake, ulikuwa kama mti wa mfumaji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha yakawa tena mapigano na Wafilisti; ndipo, Elihanani, mwana wa Yairi, alipompiga Lahami, nduguye Goliati wa Gati aliyekuwa na mkuki wenye uti kama majiti ya wafuma nguo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kulikuwa na vita tena na Wafilisti; na Elhanani, mwana wa Yairi akamwua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mti wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kukatokea tena vita na Wafilistini. Naye Elihanani mwana wa Yairi akamwua Lami ndugu ya Goliati wa muji wa Gati ambaye mupini wa mukuki wake ulikuwa kama muti wa mufumaji wa nguo.