1 Chronicles 21:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Njaa ya miaka mitatu, au miezi mitatu ya maangamizi kutokana na maadui zako ambapo upanga wa maadui zako utakushinda; au siku tatu ambapo Mwenyezi-Mungu atawashambulia kwa upanga wake, awaletee maradhi mabaya nchini, na malaika wake apite kuwaangamiza katika nchi nzima ya Israeli. Sasa amua, ni jibu lipi nitakalompa yeye aliyenituma.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
miaka mitatu ya njaa; au miezi mitatu ya kushindwa na adui zako, ukipatwa na panga zao; au siku tatu za upanga wa Mwenyezi Mungu: siku tatu za tauni katika nchi na malaika wa Mwenyezi Mungu akiangamiza kila mahali katika Israeli.’ Sasa basi, amua jinsi nitakavyomjibu yeye aliyenituma.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
miaka mitatu ya njaa; au miezi mitatu kuangamia mbele ya adui zako, ukipatwa na upanga wa watesi wako; au siku tatu upanga wa Bwana, yaani tauni katika nchi, na malaika wa Bwana akiharibu kati ya mipaka yote ya Israeli. Haya basi ufikiri ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
njaa ya miaka mitatu, au miezi mitatu ya maangamizi kutokana na maadui zako ambapo upanga wa maadui zako utakushinda; au siku tatu ambapo Mwenyezi-Mungu atawashambulia kwa upanga wake, awaletee maradhi mabaya nchini, na malaika wake apite kuwaangamiza katika nchi nzima ya Israeli. Sasa amua, ni jibu lipi nitakalompa yeye aliyenituma.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
miaka mitatu ya njaa, au miezi mitatu ya kushindwa na adui zako, ukipatwa na upanga wao, au siku tatu za upanga wa BWANA, yaani, siku tatu za tauni katika nchi na malaika wa BWANA akiangamiza kila mahali katika Israeli.’ Sasa basi, amua jinsi nitakavyomjibu yeye aliyenituma.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
miaka mitatu ya njaa, au miezi mitatu ya kushindwa na adui zako, ukipatwa na upanga wao, au siku tatu za upanga wa bwana, yaani, siku tatu za tauni katika nchi na malaika wa bwana akiangamiza kila mahali katika Israeli.’ Sasa basi, amua jinsi nitakavyomjibu yeye aliyenituma.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
miaka mitatu ya njaa; au miezi mitatu kuangamia mbele ya adui zako, ukipatwa na upanga wa watesi wako; au siku tatu upanga wa BWANA, yaani tauni katika nchi, na malaika wa BWANA akiharibu kati ya mipaka yote ya Israeli. Haya basi ufikiri ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Njaa ya miaka mitatu, au miezi mitatu ya maangamizi kutokana na maadui zako ambapo upanga wa maadui zako utakushinda; au siku tatu ambapo Mwenyezi-Mungu atawashambulia kwa upanga wake, awaletee maradhi mabaya nchini, na malaika wake apite kuwaangamiza katika nchi nzima ya Israeli. Sasa amua, ni jibu lipi nitakalompa yeye aliyenituma.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Unataka miaka mitatu ya njaa? au unataka kukimbizwa miezi mitatu machoni pao wakusongao, panga za adui zako zikikupata? au unataka, upanga wa Bwana na ugonjwa mbaya uuao upite katika nchi hii, malaika wa Bwana akifanya maovu katika mipaka yote ya Waisiraeli? Sasa tafuta, uone nitakayomjibu aliyenituma!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
miaka mitatu ya njaa; au miezi mitatu kuangamia mbele ya adui zako, ukipatwa na upanga wa watesi wako; au siku tatu upanga wa BWANA, yaani tauni katika nchi, na malaika wa BWANA akiharibu kati ya mipaka yote ya Israeli. Haya basi ufikiri ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
njaa ya miaka mitatu; au miezi mitatu ya maangamizi kutokana na waadui zako ambapo upanga wa waadui zako utakushinda; au siku tatu ambazo Yawe atawashambulia kwa upanga wake, awaletee ugonjwa mukali katika inchi, na malaika wake apite kuwaangamiza katika inchi nzima ya Israeli. Sasa amua. Ni jibu gani nitakalomupa yeye aliyenituma.’ ”