1 Chronicles 21:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi akamjibu Gadi, “Nimeingia katika mashaka makubwa! Lakini afadhali niadhibiwe na Mwenyezi-Mungu kwani yeye ana huruma sana. Ila nisianguke katika mkono wa mwanadamu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akamwambia Gadi, “Ninayo mahangaiko makubwa. Mimi na nianguke mikononi mwa Mwenyezi Mungu, kwa maana rehema zake ni kuu mno, lakini usiniache niangukie mikononi mwa wanadamu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na nianguke katika mkono wa Bwana; kwa kuwa rehema zake ni nyingi sana; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi akamjibu Gadi, “Nimeingia katika mashaka makubwa! Lakini afadhali niadhibiwe na Mwenyezi-Mungu kwani yeye ana huruma sana. Ila nisianguke katika mkono wa mwanadamu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akamwambia Gadi, “Ninayo mahangaiko makubwa. Mimi na nianguke mikononi mwa BWANA kwa sababu rehema zake ni kuu mno, lakini usiniache niangukie mikononi mwa wanadamu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akamwambia Gadi, “Ninayo mahangaiko makubwa. Mimi na nianguke mikononi mwa bwana kwa maana rehema zake ni kuu mno, lakini usiniache niangukie mikononi mwa wanadamu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na nianguke katika mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema zake ni nyingi sana; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi akamjibu Gadi, “Nimeingia katika mashaka makubwa! Lakini afadhali niadhibiwe na Mwenyezi-Mungu kwani yeye ana huruma sana. Ila nisianguke katika mkono wa mwanadamu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akamwambia Gadi: Nimesongeka sana, lakini na nijitupe mkononi mwake Bwana, kwani huruma zake ni nyingi mno nisijitupe mikononi mwa watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na nianguke katika mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema zake ni nyingi sana; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akamujibu Gadi: “Nimeingia katika mashaka makubwa! Lakini afazali niazibiwe na Yawe maana yeye ana huruma sana. Lakini nisianguke katika mukono wa mwanadamu.”