1 Chronicles 21:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu Mungu akatuma malaika aende kuuharibu Yerusalemu; lakini kabla hajafanya hivyo, Mwenyezi-Mungu akageuza nia yake na kumwambia malaika huyo aliyetekeleza maangamizi, “Basi, yatosha!” Malaika alikuwa amesimama karibu na uwanja wa kupuria nafaka wa Ornani, Myebusi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu akapeleka malaika kuangamiza Yerusalemu. Lakini malaika alipokuwa akifanya hivyo, Mwenyezi Mungu akaona na akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anaangamiza watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa Mwenyezi Mungu alikuwa amesimama katika sakafu ya kupuria nafaka ya Arauna Myebusi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Mungu akatuma malaika aende Yerusalemu ili auangamize; naye alipokuwa tayari kuangamiza, Bwana akatazama, akaghairi katika mabaya, akamwambia malaika aharibuye, Basi yatosha; sasa ulegeze mkono wako. Naye malaika wa Bwana akasimama karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu Mungu akatuma malaika aende kuuharibu Yerusalemu; lakini kabla hajafanya hivyo, Mwenyezi-Mungu akageuza nia yake na kumwambia malaika huyo aliyetekeleza maangamizi, “Basi, yatosha!” Malaika alikuwa amesimama karibu na uwanja wa kupuria nafaka wa Ornani, Myebusi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu akapeleka malaika kuangamiza Yerusalemu. Lakini malaika alipokuwa akifanya hivyo, BWANA akaona na akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anaangamiza watu, “Yatosha! Sasa rudisha mkono wako.” Wakati huu huyu malaika wa BWANA alikuwa amesimama katika uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna, Myebusi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu akapeleka malaika kuangamiza Yerusalemu. Lakini malaika alipokuwa akifanya hivyo, bwana akaona na akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anaangamiza watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa bwana alikuwa amesimama katika sakafu ya kupuria nafaka ya Arauna Myebusi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Mungu akatuma malaika aende Yerusalemu ili auangamize; naye alipokuwa tayari kuangamiza, BWANA akatazama, akaghairi katika mabaya, akamwambia malaika aharibuye, Basi yatosha; sasa ulegeze mkono wako. Naye malaika wa BWANA akasimama karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu Mungu akatuma malaika aende kuuharibu Yerusalemu; lakini kabla hajafanya hivyo, Mwenyezi-Mungu akageuza nia yake na kumwambia malaika huyo aliyetekeleza maangamizi, “Basi, yatosha!” Malaika alikuwa amesimama karibu na uwanja wa kupuria nafaka wa Ornani, Myebusi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mungu akamtuma malaika wake namo Yerusalemu, afanye humo namo maovu yake; lakini Bwana alipoyaona hayo maovu, aliyoyafanya, akageuza moyo kwa ajili ya huo ubaya, akamwambia yule malaika aliyeangamiza: Sasa inatosha, ulegeze mkono wako! Naye yule malaika wa Bwana alikuwa akisimama penye kupuria ngano pa Myebusi Ornani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Mungu akatuma malaika aende Yerusalemu ili auangamize; naye alipokuwa tayari kuangamiza, BWANA akatazama, akaghairi katika mabaya, akamwambia malaika aharibuye, Basi yatosha; sasa ulegeze mkono wako. Naye malaika wa BWANA akasimama karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Mungu akatuma malaika aende kuharibu Yerusalema. Lakini mbele hajafanya vile, Yawe akageuza nia yake na kumwambia malaika yule aliyetimiza maangamizi: “Basi, inatosha!” Malaika alikuwa amesimama karibu na uwanja wa kupepetea ngano wa Ornani wa kabila ya Yebusi.