1 Chronicles 21:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi akainua macho yake, akamwona huyo malaika wa Mwenyezi-Mungu amesimama kati ya mbingu na dunia, naye ameunyosha upanga wake juu ya Yerusalemu tayari kuuangamiza. Hapo Daudi na wazee wote walikuwa wamevaa mavazi ya gunia, wakaanguka kifudifudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akayainua macho yake, akamwona huyo malaika wa Mwenyezi Mungu akiwa amesimama katikati ya mbingu na dunia, naye ameunyoosha upanga wake juu ya Yerusalemu tayari kuangamiza. Kisha Daudi na wazee, waliokuwa wamevaa gunia, wakaanguka kifudifudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daudi akainua macho yake, akamwona huyo malaika wa Bwana amesimama kati ya nchi na mbingu, naye alikuwa na upanga wazi mkononi, umenyoshwa juu ya Yerusakmu. Ndipo Daudi na wazee wakaanguka kifulifuli, nao wamevaa nguo za magunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi akainua macho yake, akamwona huyo malaika wa Mwenyezi-Mungu amesimama kati ya mbingu na dunia, naye ameunyosha upanga wake juu ya Yerusalemu tayari kuuangamiza. Hapo Daudi na wazee wote walikuwa wamevaa mavazi ya gunia, wakaanguka kifudifudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akayainua macho yake akamwona huyo malaika wa BWANA akiwa amesimama katikati ya mbingu na dunia, naye ameunyosha upanga wake juu ya Yerusalemu tayari kuangamiza. Kisha Daudi na wazee, waliokuwa wamevaa nguo za gunia, wakaanguka kifudifudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akayainua macho yake akamwona huyo malaika wa bwana akiwa amesimama katikati ya mbingu na dunia, naye ameunyoosha upanga wake juu ya Yerusalemu tayari kuangamiza. Kisha Daudi na wazee, waliokuwa wamevaa nguo za gunia, wakaanguka kifudifudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daudi akainua macho yake, akamwona huyo malaika wa BWANA amesimama kati ya nchi na mbingu, naye alikuwa na upanga wazi mkononi, umenyoshwa juu ya Yerusalemu. Ndipo Daudi na wazee wakaanguka kifudifudi, nao wamevaa nguo za magunia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi akainua macho yake, akamwona huyo malaika wa Mwenyezi-Mungu amesimama kati ya mbingu na dunia, naye ameunyosha upanga wake juu ya Yerusalemu tayari kuuangamiza. Hapo Daudi na wazee wote walikuwa wamevaa mavazi ya gunia, wakaanguka kifudifudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi alipoyainua macho yake, akamwona malaika wa Bwana, akisimama kati ya nchi na ya mbingu, nao upanga uliochomolewa ulikuwa mkononi mwake kuuelekea Yerusalemu; ndipo, Dawidi na wazee waliokuwa wamevaa magunia walipoanguka kifudifudi,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daudi akainua macho yake, akamwona huyo malaika wa BWANA amesimama kati ya nchi na mbingu, naye alikuwa na upanga wazi mkononi, umenyoshwa juu ya Yerusakmu. Ndipo Daudi na wazee wakaanguka kifulifuli, nao wamevaa nguo za magunia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akainua macho yake, akamwona yule malaika wa Yawe akisimama kati ya mbingu na dunia, naye akiinua upanga wake juu ya Yerusalema tayari kuangamiza. Halafu Daudi na wazee wote walikuwa wakivaa nguo ya gunia, wakaanguka uso mpaka chini.