1 Chronicles 21:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwamuru Gadi amwambie Daudi aende amjengee Mwenyezi-Mungu madhabahu, katika kiwanja cha kupuria nafaka cha Ornani Myebusi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha malaika wa Mwenyezi Mungu akamwamuru Gadi amwambie Daudi apande na kumjengea Mwenyezi Mungu madhabahu kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Arauna Myebusi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo huyo malaika wa Bwana akamwamuru Gadi kwamba amwambie Daudi, ya kuwa Daudi akwee, akamwinulie Bwana madhabahu katika kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwamuru Gadi amwambie Daudi aende amjengee Mwenyezi-Mungu madhabahu, katika kiwanja cha kupuria nafaka cha Ornani Myebusi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha malaika wa BWANA akamwamuru Gadi amwambie Daudi apande na kumjengea BWANA madhabahu katika uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna, Myebusi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha malaika wa bwana akamwamuru Gadi amwambie Daudi apande na kumjengea bwana madhabahu kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Arauna Myebusi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo huyo malaika wa BWANA akamwamuru Gadi kwamba amwambie Daudi, ya kuwa Daudi akwee, akamwinulie BWANA madhabahu katika kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwamuru Gadi amwambie Daudi aende amjengee Mwenyezi-Mungu madhabahu, katika kiwanja cha kupuria nafaka cha Ornani Myebusi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, malaika wa Bwana alipomwambia Gadi, amwambie Dawidi, Dawidi apande kutengeneza pa kumtambikia Bwana papo hapo penye kupuria ngano pa Myebusi Ornani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo huyo malaika wa BWANA akamwamuru Gadi kwamba amwambie Daudi, ya kuwa Daudi akwee, akamwinulie BWANA madhabahu katika kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu malaika wa Yawe akamwamuru Gadi amwambie Daudi aende kumujengea Yawe mazabahu, katika kiwanja cha kupepetea ngano cha Ornani wa kabila ya Yebusi.