1 Chronicles 21:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi akamwambia Ornani, “Nipe nafasi ya uwanja wako wa kupuria nafaka ili nimjengee Mwenyezi-Mungu madhabahu juu yake, ili kwamba tauni ipate kuzuiliwa kwa watu. Niuzie kwa bei yake kamili.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akamwambia Arauna, “Nipatie huu uwanja wako wa kupuria nafaka, niweze kujenga madhabahu ya Mwenyezi Mungu, ili tauni ipate kukomeshwa katika watu. Niuzie kwa bei yake kamili.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Daudi akamwambia Arauna, Unipe mahali pa kiwanja hiki, ili kwamba nimjengee Bwana madhabahu hapa; kwa thamani yake kamili utanipa; ili kwamba tauni izuiliwe katika watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi akamwambia Ornani, “Nipe nafasi ya uwanja wako wa kupuria nafaka ili nimjengee Mwenyezi-Mungu madhabahu juu yake, ili kwamba tauni ipate kuzuiliwa kwa watu. Niuzie kwa bei yake kamili.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akamwambia, “Nipatie huu uwanja wako wa kupuria nafaka ili niweze kujenga madhabahu ya BWANA tauni ipate kukomeshwa katika watu. Niuzie kwa bei yake kamili.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akamwambia, “Nipatie huu uwanja wako wa kupuria nafaka ili niweze kujenga madhabahu ya bwana tauni ipate kukomeshwa katika watu. Niuzie kwa bei yake kamili.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Daudi akamwambia Arauna, Unipe mahali pa kiwanja hiki, ili kwamba nimjengee BWANA madhabahu hapa; kwa thamani yake kamili utanipa; ili kwamba tauni izuiliwe katika watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi akamwambia Ornani, “Nipe nafasi ya uwanja wako wa kupuria nafaka ili nimjengee Mwenyezi-Mungu madhabahu juu yake, ili kwamba tauni ipate kuzuiliwa kwa watu. Niuzie kwa bei yake kamili.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akamwambia Ornani: Nipe mahali hapa pa kupuria ngano, nipajenge pa kumtambikia Bwana! Nitakulipa fedha zote zipapasazo, nipe tu mahali hapa, huku kuuawa kwa watu kukomeshwe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Daudi akamwambia Arauna, Unipe mahali pa kiwanja hiki, ili kwamba nimjengee BWANA madhabahu hapa; kwa thamani yake kamili utanipa; ili kwamba tauni izuiliwe katika watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akamwambia Ornani: “Unipe nafasi ya uwanja wako wa kupepetea ngano kusudi nimujengee Yawe mazabahu juu yake, kusudi ugonjwa mukali upate kuzuiliwa katika watu. Uniuzishie kwa bei yake kamili.”