1 Chronicles 21:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Ornani akamwambia Daudi, “Kichukue kiwanja hiki, bwana wangu mfalme, na ukitumie vile unavyopenda mwenyewe. Tazama, nawatoa fahali kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, na vifaa vya kupuria kwa kuni, pamoja na ngano iwe tambiko ya nafaka. Vyote hivyo ninakupa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Arauna akamwambia Daudi, “Uchukue huo uwanja. Mfalme bwana wangu na afanye lolote analopenda. Tazama, nitatoa maksai kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, vifaa vya kupuria kuwa kuni, pamoja na ngano kwa ajili ya dhabihu ya nafaka. Natoa hivi vyote.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Arauna akamwambia Daudi, Ujitwalie, na bwana wangu mfalme na afanye yaliyo mema machoni pake; tazama, ng'ombe kwa sadaka za kuteketezwa, na vyombo vya kupuria kwa kuni, na ngano kwa sadaka ya unga, nazitoa; zote nazitoa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Ornani akamwambia Daudi, “Kichukue kiwanja hiki, bwana wangu mfalme, na ukitumie vile unavyopenda mwenyewe. Tazama, nawatoa fahali kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, na vifaa vya kupuria kwa kuni, pamoja na ngano iwe tambiko ya nafaka. Vyote hivyo ninakupa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Arauna akamwambia Daudi, “Uchukue huo uwanja. Mfalme bwana wangu na afanye lo lote analopenda. Tazama, nitatoa maksai kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, vifaa vya kupuria kuwa kuni, pamoja na ngano kwa ajili ya dhabihu ya nafaka. Natoa hivi vyote.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Arauna akamwambia Daudi, “Uchukue huo uwanja. Mfalme bwana wangu na afanye lolote analopenda. Tazama, nitatoa maksai kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, vifaa vya kupuria kuwa kuni, pamoja na ngano kwa ajili ya dhabihu ya nafaka. Natoa hivi vyote.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Arauna akamwambia Daudi, Ujitwalie, na bwana wangu mfalme na afanye yaliyo mema machoni pake; tazama, ng'ombe kwa sadaka za kuteketezwa, na vyombo vya kupuria kwa kuni, na ngano kwa sadaka ya unga, nazitoa; zote nazitoa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Ornani akamwambia Daudi, “Kichukue kiwanja hiki, bwana wangu mfalme, na ukitumie vile unavyopenda mwenyewe. Tazama, nawatoa fahali kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, na vifaa vya kupuria kwa kuni, pamoja na ngano iwe tambiko ya nafaka. Vyote hivyo ninakupa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ornani akamwambia Dawidi: Jichukulie tu! Bwana wangu mfalme na afanye, anayoyaona kuwa mema. Tazama, nakupa hawa ng'ombe kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, nayo haya magari nakupa kuwa kuni, nazo hizi ngano zote nakupa kuwa vilaji vya tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Arauna akamwambia Daudi, Ujitwalie, na bwana wangu mfalme na afanye yaliyo mema machoni pake; tazama, ng’ombe kwa sadaka za kuteketezwa, na vyombo vya kupuria kwa kuni, na ngano kwa sadaka ya unga, nazitoa; zote nazitoa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Ornani akamwambia Daudi: “Utwae kiwanja hiki, bwana wangu mufalme, na ukitumie vile unavyopenda mwenyewe. Angalia, ninawatoa ngombe dume kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, na vifaa vya kupepetea kwa kuni, pamoja na ngano ikuwe sadaka ya unga. Vyote hivyo ninakupa.”