1 Chronicles 21:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Daudi akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu mahali hapo na kumtolea sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Akamwomba Mwenyezi-Mungu, naye akakubali ombi lake kwa kuleta moto kutoka mbinguni kuiteketeza ile sadaka kwenye madhabahu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Daudi akamjengea Mwenyezi Mungu madhabahu mahali hapo, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Akamwita Mwenyezi Mungu naye Mwenyezi Mungu akajibu maombi yake kwa moto kutoka mbinguni juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Daudi akamjengea Bwana madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akamlingana Bwana; naye akamwitikia kutoka mbinguni kwa moto juu ya madhabahu hiyo ya sadaka ya kuteketezwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Daudi akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu mahali hapo na kumtolea sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Akamwomba Mwenyezi-Mungu, naye akakubali ombi lake kwa kuleta moto kutoka mbinguni kuiteketeza ile sadaka kwenye madhabahu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Daudi akamjengea BWANA madhabahu mahali hapo na kumtolea sadaka za kutekezwa na sadaka za amani. Akamwita BWANA naye BWANA akajibu maombi yake kwa moto toka mbinguni juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Daudi akamjengea bwana madhabahu mahali hapo, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Akamwita bwana naye bwana akajibu maombi yake kwa moto toka mbinguni juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Daudi akamjengea BWANA madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akamlingana BWANA; naye akamwitikia kutoka mbinguni kwa moto juu ya madhabahu hiyo ya sadaka ya kuteketezwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Daudi akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu mahali hapo na kumtolea sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Akamwomba Mwenyezi-Mungu, naye akakubali ombi lake kwa kuleta moto kutoka mbinguni kuiteketeza ile sadaka kwenye madhabahu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Dawidi akamjengea Bwana hapo mahali pa kumtambikia, akamtolea ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na vipaji vya tambiko vya kumshukuru, akamwita Bwana na kumwomba, naye akamwitikia akitoa moto mbinguni, upaangukie hapo pa kumtambikia kwa kumtolea ng'ombe za kuteketezwa nzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Daudi akamjengea BWANA madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akamlingana BWANA; naye akamwitikia kutoka mbinguni kwa moto juu ya madhabahu hiyo ya sadaka ya kuteketezwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Daudi akamujengea Yawe mazabahu pahali pale na kumutolea sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani. Akamwomba Yawe, naye akakubali maombi yake kwa kuleta moto kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka kwenye mazabahu.