1 Chronicles 21:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoabu akampelekea mfalme Daudi idadi ya watu: Katika Israeli yote, kulikuwamo wanaume 1,100,000, wenye ujuzi wa kutumia upanga; na katika Yuda kulikuwamo watu 470,000, wenye ujuzi wa kutumia upanga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yoabu akamtolea Daudi idadi ya wapiganaji: Katika Israeli yote kulikuwa na watu milioni moja na elfu mia moja ambao wangeweza kutumia upanga, wakiwemo watu elfu mia nne sabini wa Yuda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yoabu akamtolea Daudi jumla ya hesabu ya watu. Na hao wote wa Israeli walikuwa watu elfu mara elfu, na mia elfu, wenye kufuta panga; na wa Yuda watu mia nne na sabini elfu, wenye kufuta panga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoabu akampelekea mfalme Daudi idadi ya watu: katika Israeli yote, kulikuwamo wanaume 1,100,000, wenye ujuzi wa kutumia upanga; na katika Yuda kulikuwamo watu 470,000, wenye ujuzi wa kutumia upanga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yoabu akampa Daudi jumla ya idadi ya watu wanaoweza kupigana. Katika Israeli kulikuwa na watu 1,100,000 ambao wangeweza kutumia upanga na katika Yuda watu 470,000.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yoabu akampa Daudi jumla ya idadi ya watu wanaoweza kupigana. Katika Israeli kulikuwa na watu 1,100,000 ambao wangeweza kutumia upanga na katika Yuda watu 470,000.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yoabu akamtolea Daudi jumla ya hesabu ya watu. Na hao wote wa Israeli walikuwa watu milioni moja na laki moja, wenye kufuta panga; na wa Yuda watu elfu mia nne sabini (470,000), wenye kufuta panga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoabu akampelekea mfalme Daudi idadi ya watu: Katika Israeli yote, kulikuwamo wanaume 1,100,000, wenye ujuzi wa kutumia upanga; na katika Yuda kulikuwamo watu 470,000, wenye ujuzi wa kutumia upanga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo Yoabu akampasha Dawidi habari za jumla ya watu waliohesabiwa, wakawa Waisiraeli wote watu milioni moja na 100000 wenye kushika panga, nao Wayuda walikuwa watu 470000 wenye kushika panga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yoabu akamtolea Daudi jumla ya hesabu ya watu. Na hao wote wa Israeli walikuwa watu elfu mara elfu, na mia elfu, wenye kufuta panga; na wa Yuda watu mia nne na sabini elfu, wenye kufuta panga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoabu akamupelekea mufalme Daudi hesabu ya watu: katika inchi yote wa Israeli kulikuwa wanaume milioni moja na elfu mia moja, wenye ujuzi wa kutumia mapanga, na katika inchi ya Yuda kulikuwa watu elfu mia ine na makumi saba wenye kutumia mapanga.