1 Chronicles 22:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ukiwa mwangalifu, na ukizitii amri ambazo Mwenyezi-Mungu alimwagiza Mose juu ya Israeli, utastawi. Jipe moyo, uwe imara. Usiogope wala usifadhaike.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo utakapofanikiwa, ikiwa utakuwa na bidii kutii amri na sheria Mwenyezi Mungu alizompa Musa kwa ajili ya Israeli. Uwe hodari na ushujaa. Usiogope wala usikate tamaa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo utakapofanikiwa, ukiangalia kuzitenda amri, na hukumu, Bwana alizomwagizia Musa juu ya Israeli; uwe hodari, na wa moyo mkuu; usiogope wala usifadhaike.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ukiwa mwangalifu, na ukizitii amri ambazo Mwenyezi-Mungu alimwagiza Mose juu ya Israeli, utastawi. Jipe moyo, uwe imara. Usiogope wala usifadhaike.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo utakapofanikiwa, ikiwa utakuwa na bidii kutii amri na sheria BWANA alizompa Mose kwa ajili ya Israeli. Uwe hodari na ushujaa. Usiogope wala usikate tamaa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo utakapofanikiwa, ikiwa utakuwa na bidii kutii amri na sheria bwana alizompa Musa kwa ajili ya Israeli. Uwe hodari na ushujaa. Usiogope wala usikate tamaa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo utakapofanikiwa, ukiangalia kuzitenda amri, na hukumu, BWANA alizomwagizia Musa juu ya Israeli; uwe hodari, na wa moyo mkuu; usiogope wala usifadhaike.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ukiwa mwangalifu, na ukizitii amri ambazo Mwenyezi-Mungu alimwagiza Mose juu ya Israeli, utastawi. Jipe moyo, uwe imara. Usiogope wala usifadhaike.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, utakavyofanikiwa ukiyaangalia maongozi na maamuzi, Bwana aliyamwagiza Mose ya kutumia kwao Waisiraeli. Jipe moyo, upate nguvu, usiogope, wala usiingiwe na vituko!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo utakapofanikiwa, ukiangalia kuzitenda amri, na hukumu, BWANA alizomwagizia Musa juu ya Israeli; uwe hodari, na wa moyo mkuu; usiogope wala usifadhaike.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ukiwa mwangalifu, na ukitii masharti na maagizo ambayo Yawe alimwagiza Musa juu ya Israeli, utastawi. Ujipe moyo, ukuwe imara. Usiogope wala usifazaike.