1 Chronicles 22:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa juhudi kubwa, nimeiwekea akiba nyumba ya Mwenyezi-Mungu, talanta 100,000 za dhahabu, talanta 1,000,000 za fedha na idadi isiyopimika ya shaba na chuma, kwani ni nyingi sana. Nimeandaa mbao na mawe tayari. Lakini huna budi kuongezea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu: talanta elfu mia moja za dhahabu, talanta milioni moja za fedha, na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe unaweza kuviongeza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa, tazama, katika shida yangu, nimeiwekea akiba nyumba ya Bwana, talanta elfu mia za dhahabu, na talanta elfu elfu za fedha; na shaba na chuma isiyo na uzani; kwa vile zilivyo tele; miti tena na mawe nimeweka akiba, nawe utaweza kuongeza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa juhudi kubwa, nimeiwekea akiba nyumba ya Mwenyezi-Mungu, talanta 100,000 za dhahabu, talanta 1,000,000 za fedha na idadi isiyopimika ya shaba na chuma, kwani ni nyingi sana. Nimeandaa mbao na mawe tayari. Lakini huna budi kuongezea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la BWANA talanta 100,000 za dhahabu, talanta 1,000,000 za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la bwana: talanta 100,000 za dhahabu, talanta 1,000,000 za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa, tazama, katika shida yangu, nimeiwekea akiba nyumba ya BWANA, talanta laki moja za dhahabu, na talanta milioni moja za fedha; na shaba na chuma isiyo na uzani; kwa vile zilivyo tele; miti tena na mawe nimeweka akiba, nawe utaweza kuongeza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa juhudi kubwa, nimeiwekea akiba nyumba ya Mwenyezi-Mungu, talanta 100,000 za dhahabu, talanta 1,000,000 za fedha na idadi isiyopimika ya shaba na chuma, kwani ni nyingi sana. Nimeandaa mbao na mawe tayari. Lakini huna budi kuongezea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama, ingawa nimekuwa mwenye masumbuko, nyumba ya Bwana nimeiwekea vipande vya dhahabu elfu mia, ndio shilingi kama milioni 22000 na vipande vya fedha milioni moja, ndio shilingi kama milioni 12000, tena shaba na vyuma visivyopimika kwa kuwa vingi; hata miti na mawe nimeweka, lakini haya utayaongeza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa, tazama, katika shida yangu, nimeiwekea akiba nyumba ya BWANA, talanta elfu mia za dhahabu, na talanta elfu elfu za fedha; na shaba na chuma isiyo na uzani; kwa vile zilivyo tele; miti tena na mawe nimeweka akiba, nawe utaweza kuongeza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa juhudi kubwa, nimeiwekea akiba nyumba ya Yawe zaidi ya toni elfu tatu za zahabu, zaidi ya toni elfu moja za feza pamoja na shaba na chuma visivyoweza kupimwa maana ni vingi sana. Nimetayarisha mbao na mawe. Lakini utaweza kuongeza.