1 Chronicles 22:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, mtumikieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa nia na moyo wote. Shime basi! Mjengeeni Mwenyezi-Mungu mahali patakatifu ili sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu pamoja na vyombo vyote vitakatifu vitumiwavyo katika ibada, viwekwe ndani ya nyumba iliyojengwa kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa itoeni mioyo yenu na nafsi zenu katika kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Anzeni kujenga Maskani ya Bwana Mwenyezi Mungu, ili mweze kulileta Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu na vyombo vitakatifu vya Mungu katika Hekalu litakalojengwa kwa ajili ya Jina la Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa jitieni moyo na nia kumtafuta Bwana, Mungu wenu; inukeni basi, mkamjengee Bwana Mungu mahali patakatifu, ili kulileta sanduku la agano la Bwana, na vyombo vitakatifu vya Mungu, ndani ya nyumba itakayojengwa kwa ajili ya jina la Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, mtumikieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa nia na moyo wote. Shime basi! Mjengeeni Mwenyezi-Mungu mahali patakatifu ili sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu pamoja na vyombo vyote vitakatifu vitumiwavyo katika ibada, viwekwe ndani ya nyumba iliyojengwa kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa itoeni mioyo yenu na nafsi zenu katika kumtafuta BWANA Mungu wenu. Anzeni kujenga Maskani ya BWANA Mungu, ili mweze kulileta Sanduku la Agano la BWANA na vyombo vitakatifu vya Mungu katika Hekalu litakalojengwa kwa ajili ya Jina la BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa itoeni mioyo yenu na nafsi zenu katika kumtafuta bwana Mwenyezi Mungu wenu. Anzeni kujenga Maskani ya bwana Mwenyezi Mungu, ili mweze kulileta Sanduku la Agano la bwana na vyombo vitakatifu vya Mungu katika Hekalu litakalojengwa kwa ajili ya Jina la bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa jitieni moyo na nia kumtafuta BWANA, Mungu wenu; inukeni basi, mkamjengee BWANA Mungu mahali patakatifu, ili kulileta sanduku la Agano la BWANA, na vyombo vitakatifu vya Mungu, ndani ya nyumba itakayojengwa kwa ajili ya jina la BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa, mtumikieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa nia na moyo wote. Shime basi! Mjengeeni Mwenyezi-Mungu mahali patakatifu ili sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu pamoja na vyombo vyote vitakatifu vitumiwavyo katika ibada, viwekwe ndani ya nyumba iliyojengwa kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa jipeni mioyo na kuzikaza roho zenu, mmtafute Bwana Mungu wenu! Inukeni, pajengeni Patakatifu pa Bwana Mungu, mlipeleke Sanduku la Agano la Bwana na vyombo vitakatifu vya Mungu katika nyumba hiyo itakayojengewa Jina la Bwana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa jitieni moyo na nia kumtafuta BWANA, Mungu wenu; inukeni basi, mkamjengee BWANA Mungu mahali patakatifu, ili kulileta sanduku la agano la BWANA, na vyombo vitakatifu vya Mungu, ndani ya nyumba itakayojengwa kwa ajili ya jina la BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, mumutumikie Yawe, Mungu wenu, kwa nia na moyo wote. Basi mujitayarishe kumujengea Yawe pahali patakatifu kusudi Sanduku la Agano la Yawe pamoja na vyombo vyote vitakatifu vinavyotumiwa katika ibada, viwekwe ndani ya nyumba iliyojengwa kwa ajili ya Yawe.”