1 Chronicles 23:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wana wa Amramu walikuwa Aroni na Mose. Aroni aliteuliwa awe akiweka wakfu vyombo vitakatifu kabisa, pia wazawa wake daima wafukizie ubani mbele za Mwenyezi-Mungu, wakimtumikia na kuwabariki watu katika jina la Mwenyezi-Mungu milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wana wa Amramu walikuwa: Haruni na Musa. Haruni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za Mwenyezi Mungu, kuhudumu mbele zake na kubariki katika Jina la Mwenyezi Mungu milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za Bwana, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wana wa Amramu walikuwa Aroni na Mose. Aroni aliteuliwa awe akiweka wakfu vyombo vitakatifu kabisa, pia wazawa wake daima wafukizie ubani mbele za Mwenyezi-Mungu, wakimtumikia na kuwabariki watu katika jina la Mwenyezi-Mungu milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wana wa Amramu walikuwa: Aroni na Mose. Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vile vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za BWANA, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la BWANA milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wana wa Amramu walikuwa: Haruni na Musa. Haruni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za bwana, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la bwana milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za BWANA, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wana wa Amramu walikuwa Aroni na Mose. Aroni aliteuliwa awe akiweka wakfu vyombo vitakatifu kabisa, pia wazawa wake daima wafukizie ubani mbele za Mwenyezi-Mungu, wakimtumikia na kuwabariki watu katika jina la Mwenyezi-Mungu milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Amuramu walikuwa Haroni na Mose. Haroni akatengwa na kutakaswa, apatumikie Patakatifu Penyewe, yeye na wanawe kale na kale, wamvukizie Bwana kwa utumishi wao, tena wawabariki watu katika Jina lake kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za BWANA, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wana wa Amuramu walikuwa: Haruni na Musa. Haruni alichaguliwa kwa kazi inayoelekea vitu vitakatifu kabisa, hata wazao wake siku zote wafukizie ubani mbele ya Yawe, wakimutumikia na kuwabariki watu katika jina la Yawe milele.