1 Chronicles 24:19 — Compare Translations

10 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hawa waliandikishwa kulingana na kazi zao kuingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kutoa huduma, kadiri ya utaratibu waliowekewa na Aroni babu yao, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, kulingana na masharti waliyoelekezwa na Haruni baba yao, kama Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huu ndio usimamizi wao katika huduma yao, waingie nyumbani mwa Bwana kwa kadiri ya agizo lao, kwa mkono wa Haruni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyomwamuru.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hawa waliandikishwa kulingana na kazi zao kuingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kutoa huduma, kadiri ya utaratibu waliowekewa na Aroni babu yao, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la BWANA kulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kama BWANA, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la bwana kulingana na masharti waliyoelekezwa na Haruni baba yao, kama bwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huu ndio utaratibu wa zamu zao katika huduma yao, ya kuingia nyumbani mwa BWANA kwa kadiri ya agizo lao, kwa mkono wa Haruni baba yao, kama BWANA, Mungu wa Israeli, alivyomwamuru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hawa waliandikishwa kulingana na kazi zao kuingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kutoa huduma, kadiri ya utaratibu waliowekewa na Aroni babu yao, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huu ulikuwa ukuu wao katika utumishi wao wa kuingia nyumbani mwa Bwana kwa matengenezo yao, aliyoyatoa baba yao Haroni, kama Bwana Mungu wa Isiraeli alivyomwagiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huu ndio usimamizi wao katika huduma yao, waingie nyumbani mwa BWANA kwa kadiri ya agizo lao, kwa mkono wa Haruni baba yao, kama BWANA, Mungu wa Israeli, alivyomwamuru.