1 Chronicles 24:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Daudi aliwapanga wazawa wa Aroni katika makundi kufuatana na huduma zao. Alisaidiwa kufanya hivyo na Sadoki, mzawa wa Eleazari, na Ahimeleki, mzawa wa Ithamari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Haruni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawagawanya Daudi, na Sadoki wa wana wa Eleazari, na Ahimeleki wa wana wa Ithamari, katika utumishi kwa kadiri ya usimamizi wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Daudi aliwapanga wazawa wa Aroni katika makundi kufuatana na huduma zao. Alisaidiwa kufanya hivyo na Sadoki, mzawa wa Eleazari, na Ahimeleki, mzawa wa Ithamari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Aroni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Haruni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawagawanya Daudi, na Sadoki wa wana wa Eleazari, na Ahimeleki wa wana wa Ithamari, katika utumishi kwa kadiri ya huduma yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Daudi aliwapanga wazawa wa Aroni katika makundi kufuatana na huduma zao. Alisaidiwa kufanya hivyo na Sadoki, mzawa wa Eleazari, na Ahimeleki, mzawa wa Ithamari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akapatana na Sadoki aliyekuwa wa wana wa Elazari na Ahimeleki aliyekuwa wa wana wa Itamari, akawagawanya, kama walivyokuwa na ukuu katika utumishi wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawagawanya Daudi, na Sadoki wa wana wa Eleazari, na Ahimeleki wa wana wa Ithamari, katika utumishi kwa kadiri ya usimamizi wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Daudi akawapanga wana wa Haruni katika makundi kufuatana na kazi zao. Alisaidiwa kufanya hivyo na Zadoki, wa uzao wa Eleazari, na Ahimeleki, wa uzao wa Itamari.