1 Chronicles 24:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Shemaya mwana wa Nathaneli, mwandishi, aliyekuwa Mlawi, aliwaandika mbele ya mfalme Daudi, maofisa wake, kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi. Ukoo wa Eleazari ulipata kura mbili, na ukoo wa Ithamari kura moja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa mbari za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari mbari moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Shemaya mwana wa Nathaneli, mwandishi, aliyekuwa Mlawi, aliwaandika mbele ya mfalme Daudi, maofisa wake, kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi. Ukoo wa Eleazari ulipata kura mbili, na ukoo wa Ithamari kura moja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwandishi Shemeia mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi, jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa koo za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari koo moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Shemaya mwana wa Nathaneli, mwandishi, aliyekuwa Mlawi, aliwaandika mbele ya mfalme Daudi, maofisa wake, kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi. Ukoo wa Eleazari ulipata kura mbili, na ukoo wa Ithamari kura moja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Semaya, mwana wa Netaneli, aliyekuwa mwandishi wao Walawi akawaandika, mfalme na wakuu wake na mtambikaji Sadoki na Ahimeleki, mwana wa Abiatari, na wakuu wa milango ya watambikaji na Walawi wakitazama, ikawa hivi: mlango mmoja wa Elazari ukichukuliwa kwa kura, ukachukuliwa nao wa pili, kisha ukachukuliwa nao mmoja wa Itamari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa mbari za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari mbari moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Semaya mwana wa Nataneli, mwandishi, aliyekuwa Mulawi, akawaandika mbele ya mufalme Daudi, wakubwa wake, kuhani Zadoki, Ahimeleki mwana wa Abiatari na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi; ukoo wa Eleazari ukatwaliwa kwa kupiga kura mbili na ukoo wa Itamari kwa kupiga kura moja.