1 Chronicles 25:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Daudi na viongozi wa Walawi, waliwateua baadhi ya wana wa Asafu, wa Hemani, na wa Yeduthuni, kuongoza katika huduma ya kutabiri kwa kutumia vinubi, na vinanda na matoazi. Hii ndiyo orodha ya wale waliochaguliwa kuongoza ibada, pamoja na aina ya kazi iliyofanywa na kila kikundi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi, pamoja na majemadari wa jeshi, wakawatenga baadhi ya wana wa Asafu, wana wa Hemani, na wana wa Yeduthuni kwa ajili ya huduma ya kutoa unabii, wakitumia vinubi, zeze na matoazi. Hii ndiyo orodha ya watu waliofanya huduma hiyo:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena Daudi na maakida wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; hii ndiyo hesabu ya wafanya kazi sawasawa na utumishi wao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Daudi na viongozi wa Walawi, waliwateua baadhi ya wana wa Asafu, wa Hemani, na wa Yeduthuni, kuongoza katika huduma ya kutabiri kwa kutumia vinubi, na vinanda na matoazi. Hii ndiyo orodha ya wale waliochaguliwa kuongoza ibada, pamoja na aina ya kazi iliyofanywa na kila kikundi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi, pamoja na majemadari wa jeshi, wakawatenga baadhi ya wana wa Asafu, wana wa Hemani na wana wa Yeduthuni, kwa ajili ya huduma ya kutoa unabii, wakitumia vinubi, zeze na matoazi. Hii ndiyo orodha ya watu waliofanya huduma hii:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi, pamoja na majemadari wa jeshi, wakawatenga baadhi ya wana wa Asafu, wana wa Hemani na wana wa Yeduthuni, kwa ajili ya huduma ya kutoa unabii, wakitumia vinubi, zeze na matoazi. Hii ndiyo orodha ya watu waliofanya huduma hii:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena Daudi na makamanda wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; hii ndiyo hesabu ya wafanya kazi kulingana na utumishi wao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Daudi na viongozi wa Walawi, waliwateua baadhi ya wana wa Asafu, wa Hemani, na wa Yeduthuni, kuongoza katika huduma ya kutabiri kwa kutumia vinubi, na vinanda na matoazi. Hii ndiyo orodha ya wale waliochaguliwa kuongoza ibada, pamoja na aina ya kazi iliyofanywa na kila kikundi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Dawidi na wakuu wa vikosi wakawatenga kwao wana wa Asafu na kwao wa Hemani na kwao wa Yedutuni wao waliolifumbua Neno kwa kupiga mazeze na mapango na matoazi, waje kutumika hivyo. Hesabu yao walioitumikia kazi hiyo ni hii:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena Daudi na maakida wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; hii ndiyo hesabu ya wafanya kazi sawasawa na utumishi wao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Daudi na viongozi wa Walawi, wakachagua wazao wa Asafu, wa Hemani, na wa Yedutuni, kwa kuongoza katika kazi ya kutabiri kwa kutumia vinubi, na vinanda na matoazi. Haya ndiyo majina ya wale waliochaguliwa kwa kuongoza ibada, pamoja na aina ya kazi iliyofanywa na kila kikundi: