1 Chronicles 26:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mabawabu hao waligawanyika katika makundi kulingana na jamaa zao, nao pia walipangiwa kazi kwenye nyumba ya Mwenyezi-Mungu kama wale Walawi wengine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa Mwenyezi Mungu kama jamaa zao walivyokuwa nazo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika hao zilikuwa zamu za mabawabu, yaani, katika hao wakuu, wenye ulinzi sawasawa na ndugu zao, wa kutumika katika nyumba ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mabawabu hao waligawanyika katika makundi kulingana na jamaa zao, nao pia walipangiwa kazi kwenye nyumba ya Mwenyezi-Mungu kama wale Walawi wengine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa BWANA kama jamaa zao walivyokuwa nazo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa bwana kama jamaa zao walivyokuwa nazo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika hao zilikuwa zamu za mabawabu, yaani, katika hao wakuu, wenye huduma kama ndugu zao, wa kutumika katika nyumba ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mabawabu hao waligawanyika katika makundi kulingana na jamaa zao, nao pia walipangiwa kazi kwenye nyumba ya Mwenyezi-Mungu kama wale Walawi wengine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika haya mafungu ya walinda malango wakuu wao walikuwa na zamu zao za kutumika nyumbani mwa Bwana sawasawa kama ndugu zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika hao zilikuwa zamu za mabawabu, yaani, katika hao wakuu, wenye ulinzi sawasawa na ndugu zao, wa kutumika katika nyumba ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hao walinzi wa milango waligawanyika katika makundi kulingana na jamaa zao, nao vilevile walipangiwa kazi kwenye nyumba ya Yawe kama wale Walawi wengine.