1 Chronicles 26:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kura ya kuchagua wa kulinda lango la mashariki ilimwangukia Shelemia. Walipiga kura pia kwa ajili ya mwanawe Zekaria, aliyekuwa mshauri mwenye busara, ikamwangukia kura ya lango la kaskazini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia. Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe Shelemia, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kura ya mashariki ya lango ikamwangukia Meshelemia. Ndipo wakamtupia kura Zekaria mwanawe, mshauri mwenye busara; na kura yake ikamtokea ya kaskazini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kura ya kuchagua wa kulinda lango la mashariki ilimwangukia Shelemia. Walipiga kura pia kwa ajili ya mwanawe Zekaria, aliyekuwa mshauri mwenye busara, ikamwangukia kura ya lango la kaskazini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia. Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia. Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kura ya lango la mashariki ikamwangukia Meshelemia. Ndipo wakamtupia kura Zekaria mwanawe, mshauri mwenye busara; na kura yake ikamtokea ya kaskazini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kura ya kuchagua wa kulinda lango la mashariki ilimwangukia Shelemia. Walipiga kura pia kwa ajili ya mwanawe Zekaria, aliyekuwa mshauri mwenye busara, ikamwangukia kura ya lango la kaskazini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo kura ya maawioni kwa jua ikamwangukia Selemia; hata mwanawe Zakaria aliyekuwa mwenye akili za kukata mashauri wakampigia kura, nayo kura yake ikaangukia kaskazini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kura ya mashariki ya lango ikamwangukia Meshelemia. Ndipo wakamtupia kura Zekaria mwanawe, mshauri mwenye busara; na kura yake ikamtokea ya kaskazini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kura ya kuchagua wa kulinda mulango wa upande wa mashariki ikamwangukia Selemia. Wakapiga kura vilevile kwa ajili ya mwana wake Zekaria, aliyekuwa mushauri mwenye hekima, ikamwangukia kura ya mulango wa upande wa kaskazini.