1 Chronicles 26:30 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Miongoni mwa Wahebroni, Hashabia na nduguze 1,700, wote watu mashujaa walipewa wajibu wa kusimamia sehemu za Israeli zilizokuwa upande wa magharibi wa mto Yordani. Walisimamia kazi yote ya Mwenyezi-Mungu na kazi za mfalme Daudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka kwa wana wa Hebroni: Hashabia na jamaa zake, watu elfu moja na mia saba wenye uwezo, waliwajibika katika Israeli magharibi mwa Yordani kwa ajili ya kazi zote za Mwenyezi Mungu na utumishi wa mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika Wahebroni, Hashabia na nduguze, mashujaa, elfu na mia saba, walikuwa na usimamizi juu ya Israeli ng'ambo ya Yordani upande wa magharibi; kwa ajili ya kazi zote za Bwana, na kwa utumishi wa mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Miongoni mwa Wahebroni, Hashabia na nduguze 1,700, wote watu mashujaa walipewa wajibu wa kusimamia sehemu za Israeli zilizokuwa upande wa magharibi wa mto Yordani. Walisimamia kazi yote ya Mwenyezi-Mungu na kazi za mfalme Daudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka kwa wana wa Hebroni: Hashabia na jamaa zake, watu 1,700 wenye uwezo, waliwajibika katika Israeli magharibi ya Yordani kwa ajili ya kazi zote za BWANA na utumishi wa mfalme
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka kwa wana wa Hebroni: Hashabia na jamaa zake, watu 1,700 wenye uwezo, waliwajibika katika Israeli magharibi ya Yordani kwa ajili ya kazi zote za bwana na utumishi wa mfalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika Wahebroni, Hashabia na nduguze, mashujaa, elfu moja na mia saba, walikuwa na usimamizi juu ya Israeli ng'ambo ya Yordani upande wa magharibi; kwa ajili ya kazi zote za BWANA, na kwa utumishi wa mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Miongoni mwa Wahebroni, Hashabia na nduguze 1,700, wote watu mashujaa walipewa wajibu wa kusimamia sehemu za Israeli zilizokuwa upande wa magharibi wa mto Yordani. Walisimamia kazi yote ya Mwenyezi-Mungu na kazi za mfalme Daudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwao wa Heburoni waliwekwa Hasabia na ndugu zake, watu 1700 wenye nguvu, kuwaangalia Waisiraeli waliokuwako ng'ambo ya huku ya Yordani, upande wa machweoni kwa jua, wafanye kazi zote za Bwana, tena wamtumikie mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika Wahebroni, Hashabia na nduguze, mashujaa, elfu na mia saba, walikuwa na usimamizi juu ya Israeli ng’ambo ya Yordani upande wa magharibi; kwa ajili ya kazi zote za BWANA, na kwa utumishi wa mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kati ya watu wa ukoo wa Hebroni, Hasabia na wandugu zake elfu moja na mia saba, wote watu mashujaa walipewa kazi ya kusimamia sehemu za inchi ya Israeli zilizokuwa upande wa magaribi wa muto Yordani. Walisimamia kazi yote ya Yawe na kazi za mufalme Daudi.