1 Chronicles 26:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Miongoni mwa Wahebroni, Yeria alikuwa kiongozi wa koo na jamaa zote, na katika mwaka wa arubaini wa utawala wa mfalme Daudi, uchunguzi ulifanywa, na wanaume wenye uwezo mkubwa walipatikana huko Yezeri katika Gileadi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhusu wana wa Hebroni, Yeria alikuwa mkuu wao kufuatana na orodha ya jamaa yao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi, uchunguzi ulifanyika katika kumbukumbu, nao watu wenye uwezo miongoni mwa wana wa Hebroni wakapatikana huko Yazeri katika Gileadi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika Wahebroni Yeria alikuwa mkuu, yaani, wa hao Wahebroni kwa kufuata vizazi vyao kwa mbari za mababa. Katika mwaka arobaini wa kutawala kwake Daudi wakatafutwa, wakaonekana huko Yazeri ya Gileadi miongoni mwao waume mashujaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Miongoni mwa Wahebroni, Yeria alikuwa kiongozi wa koo na jamaa zote, na katika mwaka wa arubaini wa utawala wa mfalme Daudi, uchunguzi ulifanywa, na wanaume wenye uwezo mkubwa walipatikana huko Yezeri katika Gileadi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhusu wana wa Hebroni, Yeria alikuwa mkuu wao kufuatana na orodha ya jamaa yao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi uchunguzi ulifanyika katika kumbukumbu, nao watu wenye uwezo miongoni mwa wana wa Hebroni wakapatikana huko Yazeri katika Gileadi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhusu wana wa Hebroni, Yeria alikuwa mkuu wao kufuatana na orodha ya jamaa yao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi uchunguzi ulifanyika katika kumbukumbu, nao watu wenye uwezo miongoni mwa wana wa Hebroni wakapatikana huko Yazeri katika Gileadi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika Wahebroni Yeria alikuwa mkuu, yaani, wa hao Wahebroni kwa kufuata vizazi vyao kwa koo za mababa. Katika mwaka arobaini wa kutawala kwake Daudi wakatafutwa, wakaonekana huko Yazeri ya Gileadi miongoni mwao wanaume mashujaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Miongoni mwa Wahebroni, Yeria alikuwa kiongozi wa koo na jamaa zote, na katika mwaka wa arubaini wa utawala wa mfalme Daudi, uchunguzi ulifanywa, na wanaume wenye uwezo mkubwa walipatikana huko Yezeri katika Gileadi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwao wa Heburoni alikuwa naye Yeria aliyekuwa mkuu wao wa Heburoni kwa vizazi vyao na kwa milango yao; walipohesabiwa katika mwaka wa arobaini wa ufalme wa Dawidi, wakaonekana kwao mafundi wa vita wenye nguvu mle Yazeri wa Gileadi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika Wahebroni Yeria alikuwa mkuu, yaani, wa hao Wahebroni kwa kufuata vizazi vyao kwa mbari za mababa. Katika mwaka arobaini wa kutawala kwake Daudi wakatafutwa, wakaonekana huko Yazeri ya Gileadi miongoni mwao waume mashujaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kati ya watu wa ukoo wa Hebroni, Yeria alikuwa kiongozi wa ukoo na jamaa zote, na katika mwaka wa makumi ine wa utawala wa mufalme Daudi, uchunguzi ulifanywa na wanaume wenye uwezo mukubwa wakapatikana kule Yezeri katika jimbo la Gileadi.