1 Chronicles 26:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Daudi alimteua Yeriya na ndugu zake 2,700, mashujaa na viongozi wa koo, kusimamia mambo yote yaliyohusu Mungu na mfalme Daudi katika sehemu za Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, zilizokuwa mashariki ya mto Yordani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeria alikuwa na jamaa ya watu elfu mbili mia saba waliokuwa watu wenye uwezo na viongozi wa jamaa, naye Mfalme Daudi akawaweka kuangalia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila Manase kuhusu kila jambo lililomhusu Mungu na shughuli za mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na nduguze, mashujaa, walikuwa elfu mbili na mia saba, wakuu wa mbari za mababa, ambao mfalme Daudi aliwaweka wawe wasimamizi juu ya Wareubeni, na Wagadi, na nusu kabila ya Wamanase, kwa ajili ya kila neno lililomhusu Mungu, na kwa mambo ya mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Daudi alimteua Yeriya na ndugu zake 2,700, mashujaa na viongozi wa koo, kusimamia mambo yote yaliyohusu Mungu na mfalme Daudi katika sehemu za Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, zilizokuwa mashariki ya mto Yordani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeria alikuwa na jamaa ya watu 2,700 waliokuwa watu wenye uwezo na viongozi wa jamaa, Mfalme Daudi akawaweka kuangalia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila Manase kuhusu kila jambo lililomhusu Mungu na shughuli za mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeria alikuwa na jamaa ya watu 2,700 waliokuwa watu wenye uwezo na viongozi wa jamaa, naye Mfalme Daudi akawaweka kuangalia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila Manase kuhusu kila jambo lililomhusu Mungu na shughuli za mfalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na nduguze, mashujaa, walikuwa elfu mbili na mia saba, wakuu wa koo za mababa, ambao mfalme Daudi aliwaweka wawe wasimamizi juu ya Wareubeni, na Wagadi, na nusu kabila la Wamanase, kwa ajili ya kila neno lililomhusu Mungu, na kwa mambo ya mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Daudi alimteua Yeriya na ndugu zake 2,700, mashujaa na viongozi wa koo, kusimamia mambo yote yaliyohusu Mungu na mfalme Daudi katika sehemu za Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, zilizokuwa mashariki ya mto Yordani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao ndugu zake waliokuwa wenye nguvu, watu 2700, nao walikuwa wakuu wa milango. Hawa mfalme Dawidi aliwaweka kuwaangalia watu wa Rubeni na wa Gadi nao wa nusu ya shina la Manase, wafanye mambo yote ya Mungu na mambo ya mfalme yawapasayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na nduguze, mashujaa, walikuwa elfu mbili na mia saba, wakuu wa mbari za mababa, ambao mfalme Daudi aliwaweka wawe wasimamizi juu ya Wareubeni, na Wagadi, na nusu kabila ya Wamanase, kwa ajili ya kila neno lililomhusu Mungu, na kwa mambo ya mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Daudi alimuchagua Yeriya na wandugu zake elfu mbili na mia saba, mashujaa na viongozi wa ukoo, kwa kusimamia mambo yote yaliyoelekea Mungu na mufalme Daudi katika sehemu za watu wa ukoo wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, zilizokuwa upande wa mashariki wa muto Yordani.