1 Chronicles 26:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye mwanawe Shemaya alipata wana waliokuwa na mamlaka juu ya jamaa ya baba yao, kwa sababu walikuwa wanaume wenye uwezo mkubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Shemaya mwanawe Obed-Edomu pia alikuwa na wana waliokuwa viongozi katika jamaa ya baba yao, kwa sababu walikuwa watu wenye uwezo mkubwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye mwanawe Shemaya akazaliwa wana, waliomiliki juu ya mbari ya baba yao; kwa kuwa walikuwa waume mashujaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye mwanawe Shemaya alipata wana waliokuwa na mamlaka juu ya jamaa ya baba yao, kwa sababu walikuwa wanaume wenye uwezo mkubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Shemaya mwanawe pia alikuwa na wana, waliokuwa viongozi katika jamaa ya baba yao kwa sababu walikuwa watu wenye uwezo mkubwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Shemaya mwanawe pia alikuwa na wana, waliokuwa viongozi katika jamaa ya baba yao kwa sababu walikuwa watu wenye uwezo mkubwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye kwa mwanawe Shemaya wakazaliwa wana, walioongoza ukoo wa baba yao; kwa kuwa walikuwa wanaume mashujaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye mwanawe Shemaya alipata wana waliokuwa na mamlaka juu ya jamaa ya baba yao, kwa sababu walikuwa wanaume wenye uwezo mkubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mwanawe Semaya alikuwa amezaliwa wana walioitawala milango yao, kwani walikuwa waume wenye nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye mwanawe Shemaya akazaliwa wana, waliomiliki juu ya mbari ya baba yao; kwa kuwa walikuwa waume mashujaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwana wake Semaya alizaa wana. Walikuwa na mamlaka juu ya jamaa ya baba yao kwa sababu walikuwa wanaume wenye uwezo mukubwa.