1 Chronicles 27:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hii ndiyo orodha ya wakuu wa wazawa wa Israeli waliokuwa viongozi wa jamaa, na makamanda wa maelfu na mamia na maofisa wao waliomtumikia mfalme Daudi kuhusu zamu za kuingia na kutoka. Kila mwezi kila mwaka, kundi tofauti la watu 24,000 walilishika zamu ya kufanya kazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii ndiyo orodha ya Waisraeli: viongozi wa jamaa, majemadari wa maelfu, majemadari wa mamia na maafisa wao, waliomtumikia mfalme kwa lolote lililohusu vikosi vya jeshi vilivyokuwa zamu mwezi baada ya mwezi katika mwaka mzima. Kila kikosi kimoja kilikuwa na watu elfu ishirini na nne.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wana wa Israeli kwa hesabu yao, wakuu wa mbari za mababa, na maakida wa maelfu na wa mamia, na wasimamizi wao waliomtumikia mfalme, kwa neno lo lote la zamu za kuingia na za kutoka mwezi kwa mwezi, miezi yote ya mwaka, wa kila zamu, walikuwa watu ishirini na nne elfu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hii ndiyo orodha ya wakuu wa wazawa wa Israeli waliokuwa viongozi wa jamaa, na makamanda wa maelfu na mamia na maofisa wao waliomtumikia mfalme Daudi kuhusu zamu za kuingia na kutoka. Kila mwezi kila mwaka, kundi tofauti la watu 24,000 walilishika zamu ya kufanya kazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii ndiyo orodha ya watu wa Waisraeli, viongozi wa jamaa, majemadari wa maelfu, majemadari wa mamia na maafisa wao, waliomtumikia mfalme kwa lo lote lile lililohusu vikosi vya jeshi vile vilivyokuwa zamu mwezi baada ya mwezi katika mwaka mzima. Kila kikosi kimoja kilikuwa na watu 24,000.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii ndiyo orodha ya Waisraeli: viongozi wa jamaa, majemadari wa maelfu, majemadari wa mamia na maafisa wao, waliomtumikia mfalme kwa lolote lililohusu vikosi vya jeshi vilivyokuwa zamu mwezi baada ya mwezi katika mwaka mzima. Kila kikosi kimoja kilikuwa na watu 24,000.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wana wa Israeli kwa hesabu yao, wakuu wa koo za mababa, na makamanda wa maelfu na wa mamia, na wasimamizi wao waliomtumikia mfalme, kwa neno lolote la zamu za kuingia na za kutoka mwezi kwa mwezi, miezi yote ya mwaka, wa kila zamu, walikuwa watu elfu ishirini na nne.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hii ndiyo orodha ya wakuu wa wazawa wa Israeli waliokuwa viongozi wa jamaa, na makamanda wa maelfu na mamia na maofisa wao waliomtumikia mfalme Daudi kuhusu zamu za kuingia na kutoka. Kila mwezi kila mwaka, kundi tofauti la watu 24,000 walilishika zamu ya kufanya kazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hii ndiyo hesabu yao wana wa Isiraeli wakuu wa milango na wakuu wa maelfu na wa mamia nao wenye amri waliomtumikia mfalme katika mambo yote yayapasayo hayo mafungu, wakiingia, tena wakitoka mwezi kwa mwezi miezi yote ya mwaka, nalo fungu moja lilikuwa watu 24000.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wana wa Israeli kwa hesabu yao, wakuu wa mbari za mababa, na maakida wa maelfu na wa mamia, na wasimamizi wao waliomtumikia mfalme, kwa neno lo lote la zamu za kuingia na za kutoka mwezi kwa mwezi, miezi yote ya mwaka, wa kila zamu, walikuwa watu ishirini na nne elfu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli waliokuwa viongozi wa jamaa, na majemadari wa maelfu na mamia na wakubwa wao waliomutumikia mufalme Daudi juu ya zamu za kuingia na kutoka. Kila mwezi katika mwaka, kundi tofauti la watu elfu makumi mbili na ine walishika zamu ya kufanya kazi.