1 Chronicles 27:5 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kamanda wa kundi la tatu likiwa na wanajeshi 24,000 alikuwa Benaya mwana wa Yehoyada, aliyekuwa kuhani mkuu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jemadari wa kikosi cha tatu kwa mwezi wa tatu alikuwa Benaya mwana wa kuhani Yehoyada. Ndiye alikuwa mkuu wa kikosi chake kilichokuwa na watu elfu ishirini na nne.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akida wa tatu wa jeshi mwezi wa tatu alikuwa Benaya, mwana wa Yehoyada, kuhani; alikuwa mkuu, na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kamanda wa kundi la tatu likiwa na wanajeshi 24,000 alikuwa Benaya mwana wa Yehoyada, aliyekuwa kuhani mkuu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jemadari wa kikosi cha tatu, kwa mwezi wa tatu, alikuwa Benaya mwana wa Yehoyada kuhani. Yeye ndiye aliyekuwa mkuu wa kikosi chake kilichokuwa na watu 24,000.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jemadari wa kikosi cha tatu kwa mwezi wa tatu alikuwa Benaya mwana wa kuhani Yehoyada. Ndiye alikuwa mkuu wa kikosi chake kilichokuwa na watu 24,000.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kamanda wa tatu wa jeshi mwezi wa tatu alikuwa Benaya, mwana wa Yehoyada, kuhani; alikuwa mkuu, na katika zamu yake walikuwa watu elfu ishirini na nne.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kamanda wa kundi la tatu likiwa na wanajeshi 24,000 alikuwa Benaya mwana wa Yehoyada, aliyekuwa kuhani mkuu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkuu wa kikosi cha tatu cha mwezi wa tatu alikuwa Benaya, mwana wa mtambikaji Yoyada, yeye alikuwa kichwa, nalo fungu lake lilikuwa lenye watu 24000.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akida wa tatu wa jeshi mwezi wa tatu alikuwa Benaya, mwana wa Yehoyada, kuhani; alikuwa mkuu, na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.