1 Chronicles 27:7 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa wa nne akiongoza kundi la nne lenye wanajeshi 24,000, na baada yake alimfuata Zebadia mwanawe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jemadari wa nne kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli nduguye Yoabu, mwanawe Zebadia ndiye aliingia mahali pake kwenye uongozi. Kikosi chake kilikuwa na watu elfu ishirini na nne.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akida wa nne wa mwezi wa nne alikuwa Asaheli, nduguye Yoabu, na Zebadia mwanawe baada yake; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa wa nne akiongoza kundi la nne lenye wanajeshi 24,000, na baada yake alimfuata Zebadia mwanawe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jemadari wa nne, kwa mwezi wa nne, alikuwa Asaheli nduguye Yoabu, mwanawe Zebadia ndiye aliyeingia mahali pake kwenye uongozi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jemadari wa nne kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli nduguye Yoabu, mwanawe Zebadia ndiye aliingia mahali pake kwenye uongozi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kamanda wa nne wa mwezi wa nne alikuwa Asaheli, nduguye Yoabu, na Zebadia mwanawe baada yake; na katika zamu yake walikuwa watu elfu ishirini na nne.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa wa nne akiongoza kundi la nne lenye wanajeshi 24,000, na baada yake alimfuata Zebadia mwanawe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkuu wa nne wa mwezi wa nne alikuwa Asaheli, ndugu yake Yoabu, naye mwanawe Zebadia alimfuata. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akida wa nne wa mwezi wa nne alikuwa Asaheli, nduguye Yoabu, na Zebadia mwanawe baada yake; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.