1 Chronicles 28:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Daudi akawakusanya huko Yerusalemu wakuu wote wa Israeli: Wa makabila, majemadari na vikosi waliomtumikia mfalme, makamanda wa maelfu, makamanda wa mamia, wasimamizi wa mali zote na ng'ombe wote wa mfalme, na wanawe pamoja na maofisa wa ikulu, mashujaa na askari wote mashuhuri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akawaita maafisa wote wa Israeli wakusanyike huko Yerusalemu: yaani maafisa walio juu ya makabila, majemadari wa vikosi katika utumishi wa mfalme, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, maafisa wanaosimamia mali yote na mifugo ya mfalme na wanawe, wakiwemo maafisa wa jumba la kifalme, mashujaa na wapiganaji hodari wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Daudi akawakusanya huko Yerusalemu wakuu wote wa Israeli, wakuu wa kabila, na maakida wa vikosi wenye kumtumikia mfalme kwa zamu, na maakida wa maelfu, na maakida wa mamia, na wenye kutawala juu ya mali na milki za mfalme, na za wanawe, pamoja na matowashi, na mashujaa, naam, waume mashujaa wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Daudi akawakusanya huko Yerusalemu wakuu wote wa Israeli: wa makabila, majemadari na vikosi waliomtumikia mfalme, makamanda wa maelfu, makamanda wa mamia, wasimamizi wa mali zote na ng'ombe wote wa mfalme, na wanawe pamoja na maofisa wa ikulu, mashujaa na askari wote mashuhuri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akawaita maafisa wote wa Israeli wakusanyike huko Yerusalemu: yaani, maafisa walio juu ya makabila, majemadari wa vikosi katika utumishi wa mfalme, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, maafisa wanaosimamia mali zote na mifugo ya mfalme na wanawe, wakiwemo maafisa wa jumba la kifalme, mashujaa na maaskari wote walio hodari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akawaita maafisa wote wa Israeli wakusanyike huko Yerusalemu: yaani, maafisa walio juu ya makabila, majemadari wa vikosi katika utumishi wa mfalme, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, maafisa wanaosimamia mali zote na mifugo ya mfalme na wanawe, wakiwemo maafisa wa jumba la kifalme, mashujaa na askari wote walio hodari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Daudi akawakusanya huko Yerusalemu wakuu wote wa Israeli, wakuu wa kabila, na makamanda wa vikosi wenye kumtumikia mfalme kwa zamu, na makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, na wenye kutawala juu ya mali na milki za mfalme, na za wanawe, pamoja na matowashi, na mashujaa, naam, wanaume mashujaa wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Daudi akawakusanya huko Yerusalemu wakuu wote wa Israeli: Wa makabila, majemadari na vikosi waliomtumikia mfalme, makamanda wa maelfu, makamanda wa mamia, wasimamizi wa mali zote na ng'ombe wote wa mfalme, na wanawe pamoja na maofisa wa ikulu, mashujaa na askari wote mashuhuri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akawakusanya Yerusalemu wakuu wote wa Waisiraeli, wakuu wa mashina na wakuu wa mafungu yaliyomtumikia mfalme na wakuu wa maelfu na wakuu wa mamia na wakuu wa mali na wa mapato yote ya mfalme na wanawe pamoja na watumishi wa nyumbani na mafundi wa vita nao wote waliokuwa waume wenye nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Daudi akawakusanya huko Yerusalemu wakuu wote wa Israeli, wakuu wa kabila, na maakida wa vikosi wenye kumtumikia mfalme kwa zamu, na maakida wa maelfu, na maakida wa mamia, na wenye kutawala juu ya mali na milki za mfalme, na za wanawe, pamoja na matowashi, na mashujaa, naam, waume mashujaa wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Daudi akakusanya kule Yerusalema wakubwa wote wa Waisraeli: wa makabila, majemadari na vikundi waliomutumikia mufalme, wakubwa wa maelfu na mamia, wasimamizi wa mali yote, ya ngombe wote wa mufalme na wana wake pamoja na wakubwa wa nyumba ya kifalme, mashujaa na waaskari wenye heshima.