1 Chronicles 28:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Daudi akampa Solomoni mwanawe ramani ya majengo yote ya hekalu, nyumba zake, hazina zake, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kiti cha rehema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Daudi akampa Sulemani mwanawe kielelezo kwa ajili ya ukumbi wa Hekalu, nyumba zake, vyumba vyake vya hazina, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kufanyia upatanisho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Daudi akampa Sulemani mwanawe mfano wa ukumbi wa hekalu, na nyumba zake, na hazina zake, na orofa zake, na vyumba vyake vya ndani, na mahali pa kiti cha rehema;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Daudi akampa Solomoni mwanawe ramani ya majengo yote ya hekalu, nyumba zake, hazina zake, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kiti cha rehema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Daudi akampa mwanawe kielelezo kwa ajili ya ukumbi wa Hekalu, nyumba zake, vyumba vyake vya hazina, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kufanyia upatanisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Daudi akampa Sulemani mwanawe kielelezo kwa ajili ya ukumbi wa Hekalu, nyumba zake, vyumba vyake vya hazina, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kufanyia upatanisho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Daudi akampa Sulemani mwanawe mfano wa ukumbi wa hekalu, na nyumba zake, na hazina zake, na ghorofa zake, na vyumba vyake vya ndani, na mahali pa kiti cha rehema;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Daudi akampa Solomoni mwanawe ramani ya majengo yote ya hekalu, nyumba zake, hazina zake, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kiti cha rehema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Dawidi akampa mwanawe salomo mfano wa ukumbi na wa nyumba zake na wa vyumba vyake vya vilimbiko na wa vyumba vya juu na wa vyumba vya ndani na wa nyumba ya kupatia upozi,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Daudi akampa Sulemani mwanawe mfano wa ukumbi wa hekalu, na nyumba zake, na hazina zake, na orofa zake, na vyumba vyake vya ndani, na mahali pa kiti cha rehema;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Daudi akamupa Solomono mwana wake mufano wa majengo yote ya hekalu, nyumba zake, hazina zake, gorofi zake, vyumba vyake vya ndani na pahali pa kiti cha rehema.