1 Chronicles 28:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makuhani na Walawi wamekwisha pangiwa kazi watakazofanya katika nyumba ya Mungu. Wafanyakazi wenye ujuzi wa kila aina watakuwa tayari kabisa kukusaidia, na watu wote pamoja na viongozi wao watakuwa chini ya amri yako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Migawanyo ya makuhani na Walawi iko tayari kwa ajili ya kazi yote katika Hekalu la Mungu, naye kila mtu mwenye moyo wa kujitolea, aliye na ustadi katika aina yoyote ya ufundi, atakusaidia katika kazi yote. Maafisa na watu wote watatii kila agizo lako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, hizo zamu za makuhani na Walawi ziko, kwa utumishi wote wa nyumba ya Mungu; nao watakuwapo pamoja nawe kwa kazi ya kila namna, kila mtu mwenye hiari, aliye stadi kwa utumishi wo wote; tena maakida na watu wote watakuwa chini ya amri yako kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makuhani na Walawi wamekwisha pangiwa kazi watakazofanya katika nyumba ya Mungu. Wafanyakazi wenye ujuzi wa kila aina watakuwa tayari kabisa kukusaidia, na watu wote pamoja na viongozi wao watakuwa chini ya amri yako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Migawanyo ya makuhani na Walawi iko tayari kwa ajili ya kazi yote katika Hekalu la Mungu, naye kila mtu mwenye moyo wa kupenda mwenye ustadi katika aina yo yote ya ufundi atakusaidia katika kazi yote. Maafisa na watu wote watatii kila agizo lako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Migawanyo ya makuhani na Walawi iko tayari kwa ajili ya kazi yote katika Hekalu la Mungu, naye kila mtu mwenye moyo wa kupenda mwenye ustadi katika aina yoyote ya ufundi atakusaidia katika kazi yote. Maafisa na watu wote watatii kila agizo lako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, hizo zamu za makuhani na Walawi ziko, kwa utumishi wote wa nyumba ya Mungu; nao watakuwapo pamoja nawe kwa kazi ya kila namna, kila mtu mwenye hiari, aliye stadi kwa utumishi wowote; tena maofisa na watu wote watakuwa chini ya amri yako kabisa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makuhani na Walawi wamekwisha pangiwa kazi watakazofanya katika nyumba ya Mungu. Wafanyakazi wenye ujuzi wa kila aina watakuwa tayari kabisa kukusaidia, na watu wote pamoja na viongozi wao watakuwa chini ya amri yako.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama! Yako mafungu ya watambikaji na ya Walawi wa kuufanya utumishi wote wa hiyo nyumba ya Mungu, tena unao mafundi wa kila kazi wanaotaka kukusaidia kwa moyo, nao huujua kweli huo utumishi wote, hata wakuu na watu wote watakutii yote, utakayowaambia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, hizo zamu za makuhani na Walawi ziko, kwa utumishi wote wa nyumba ya Mungu; nao watakuwapo pamoja nawe kwa kazi ya kila namna, kila mtu mwenye hiari, aliye stadi kwa utumishi wo wote; tena maakida na watu wote watakuwa chini ya amri yako kabisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makuhani na Walawi wamekwisha kupangiwa kazi watakazofanya katika nyumba ya Mungu. Watumishi wenye ujuzi wa kila aina watakuwa tayari kabisa kukusaidia, na watu wote pamoja na viongozi wao watakuwa chini ya mamlaka yako.”