1 Chronicles 28:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli alinichagua mimi miongoni mwa jamaa ya baba yangu kuwa mfalme wa Israeli milele. Alilichagua kabila la Yuda liongoze; na kutokana na kabila hilo, aliichagua jamaa ya baba yangu, na miongoni mwa wana wa baba yangu, alipendezwa nami na kuniweka niwe mfalme wa Israeli yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hata hivyo, Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, alinichagua mimi kutoka jamaa zangu wote niwe mfalme juu ya Israeli milele. Alimchagua Yuda kuwa kiongozi, na kutoka nyumba ya Yuda akaichagua jamaa yangu, na kutoka wana wa baba yangu ikampendeza kunifanya niwe mfalme juu ya Israeli yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini Bwana, Mungu wa Israeli, alinichagua katika nyumba yote ya babangu kuwa mfalme juu ya Israeli milele, kwa kuwa amemchagua Yuda awe mkuu; na katika nyumba ya Yuda, alichagua nyumba ya babangu, na miongoni mwa wana wa babangu, aliniridhia mimi ili kunitawaza niwe mfalme juu ya Israeli wote;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli alinichagua mimi miongoni mwa jamaa ya baba yangu kuwa mfalme wa Israeli milele. Alilichagua kabila la Yuda liongoze; na kutokana na kabila hilo, aliichagua jamaa ya baba yangu, na miongoni mwa wana wa baba yangu, alipendezwa nami na kuniweka niwe mfalme wa Israeli yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hata hivyo BWANA, Mungu wa Israeli, alinichagua mimi kutoka jamaa yangu yote niwe mfalme juu ya Israeli milele. Alimchagua Yuda kuwa kiongozi na kutoka katika nyumba ya Yuda akaichagua jamaa yangu na kutoka katika wana wa baba yangu ikampendeza kunifanya niwe mfalme juu ya Israeli yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hata hivyo, bwana, Mungu wa Israeli, alinichagua mimi kutoka jamaa yangu yote niwe mfalme juu ya Israeli milele. Alimchagua Yuda kuwa kiongozi na kutoka nyumba ya Yuda akaichagua jamaa yangu na kutoka wana wa baba yangu ikampendeza kunifanya niwe mfalme juu ya Israeli yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Walakini BWANA, Mungu wa Israeli, alinichagua katika nyumba yote ya babangu kuwa mfalme juu ya Israeli milele, kwa kuwa amemchagua Yuda awe mkuu; na katika nyumba ya Yuda, alichagua nyumba ya babangu, na miongoni mwa wana wa babangu, aliniridhia mimi ili kunitawaza niwe mfalme juu ya Israeli wote;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli alinichagua mimi miongoni mwa jamaa ya baba yangu kuwa mfalme wa Israeli milele. Alilichagua kabila la Yuda liongoze; na kutokana na kabila hilo, aliichagua jamaa ya baba yangu, na miongoni mwa wana wa baba yangu, alipendezwa nami na kuniweka niwe mfalme wa Israeli yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Bwana Mungu wa Isiraeli alinichagua katika mlango wote wa baba yangu, niwe mfalme wa Waisiraeli kale na kale, kwani alimchagua Yuda, awe mkubwa, namo mlangoni mwa Yuda akauchagua mlango wa baba yangu, namo katika wana wa baba yangu akapendezwa kunifanya mfalme wa Waisiraeli wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini BWANA, Mungu wa Israeli, alinichagua katika nyumba yote ya babangu kuwa mfalme juu ya Israeli milele, kwa kuwa amemchagua Yuda awe mkuu; na katika nyumba ya Yuda, alichagua nyumba ya babangu, na miongoni mwa wana wa babangu, aliniridhia mimi ili kunitawaza niwe mfalme juu ya Israeli wote;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yawe, Mungu wa Israeli, alinichagua mimi kati ya jamaa ya baba yangu kuwa mufalme wa Israeli kwa milele. Alichagua kabila la Yuda kusudi liongozeke; na kutokana na kabila lile, alichagua jamaa ya baba yangu, na kati ya wana wa baba yangu, alipendezwa nami na kuniweka nikuwe mufalme wa Israeli yote.