1 Chronicles 28:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Basi sasa, mbele ya kusanyiko hili la Waisraeli wote, jumuiya ya watu wa Mwenyezi-Mungu, na mbele ya Mungu wetu, angalieni mzishike amri zote za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ili mwendelee kuimiliki nchi hii nzuri, na kuwarithisha wazawa wenu baada yenu, hata milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hivyo basi ninawaagiza mbele za Israeli yote na kusanyiko hili la Mwenyezi Mungu, naye Mungu wetu akiwa anasikia: Kuweni na bidii kuzifuata amri za Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ili mpate kumiliki nchi hii nzuri, na kuwaachia wana wenu kuwa urithi milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa, machoni pa Israeli wote, hilo kusanyiko la Bwana, na masikioni pa Mungu wetu, angalieni na kuzitafuta amri zote za Bwana, Mungu wenu, ili mpate kuimiliki nchi hii njema, na kuwarithisha wana wenu baada yenu hata milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Basi sasa, mbele ya kusanyiko hili la Waisraeli wote, jumuiya ya watu wa Mwenyezi-Mungu, na mbele ya Mungu wetu, angalieni mzishike amri zote za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ili mwendelee kuimiliki nchi hii nzuri, na kuwarithisha wazawa wenu baada yenu, hata milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hivyo basi ninawaagiza mbele za Israeli yote na kusanyiko hili la BWANA naye Mungu wetu akiwa anasikia: Iweni na bidii kuzifuata amri za BWANA Mungu wenu, ili mpate kumiliki nchi hii nzuri na kuwaachia wana wenu kuwa urithi milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hivyo basi ninawaagiza mbele za Israeli yote na kusanyiko hili la bwana naye Mungu wetu akiwa anasikia: Kuweni na bidii kuzifuata amri za bwana Mwenyezi Mungu wenu, ili mpate kumiliki nchi hii nzuri na kuwaachia wana wenu kuwa urithi milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa, machoni pa Israeli wote, hilo kusanyiko la BWANA, na masikioni pa Mungu wetu, shikeni na kuzifuata amri zote za BWANA, Mungu wenu, ili mpate kuimiliki nchi hii njema, na kuwarithisha wana wenu baada yenu hata milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Basi sasa, mbele ya kusanyiko hili la Waisraeli wote, jumuiya ya watu wa Mwenyezi-Mungu, na mbele ya Mungu wetu, angalieni mzishike amri zote za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ili mwendelee kuimiliki nchi hii nzuri, na kuwarithisha wazawa wenu baada yenu, hata milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa machoni pao Waisiraeli wote walio mkutano wa Bwana namo masikioni pake Mungu wetu ninawaonya: Yaangalieni na kuyatafuta maagizo yote ya Bwana Mungu wenu, mpate kuishika nchi hii njema, iwe yenu, kisha mwiachie wana wenu watakaokuwa nyuma yenu, iwe fungu lao kale na kale!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa, machoni pa Israeli wote, hilo kusanyiko la BWANA, na masikioni pa Mungu wetu, angalieni na kuzitafuta amri zote za BWANA, Mungu wenu, ili mpate kuimiliki nchi hii njema, na kuwarithisha wana wenu baada yenu hata milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Basi sasa, mbele ya kusanyiko hili la Waisraeli wote, taifa la watu wa Yawe, na mbele ya Mungu wetu, muangalie na mushike amri zote za Yawe, Mungu wenu, kusudi muendelee kurizi inchi hii nzuri, na kuwarizisha wazao wenu nyuma yenu, hata milele.