1 Chronicles 28:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nawe Solomoni mwanangu, umjue Mungu wa baba yako, na umtumikie kwa moyo wako wote na kwa nia thabiti; yeye Mwenyezi-Mungu huchunguza mioyo na anafahamu mipango na fikira za binadamu. Ukimtafuta yeye, utamwona; lakini ukimwacha, atakutupilia mbali milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nawe Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa kujitoa kwa moyo wote na kwa nia ya kumkubali, kwa maana Mwenyezi Mungu huuchunguza kila moyo na kujua kila kusudi la kila fikira. Ukimtafuta, ataonekana kwako; bali ukimwacha, yeye atakukataa milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa Bwana hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nawe Solomoni mwanangu, umjue Mungu wa baba yako, na umtumikie kwa moyo wako wote na kwa nia thabiti; yeye Mwenyezi-Mungu huchunguza mioyo na anafahamu mipango na fikira za binadamu. Ukimtafuta yeye, utamwona; lakini ukimwacha, atakutupilia mbali milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nawe Solomoni mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa kujitoa kwa moyo wote na kwa nia ya kumkubali, kwa maana BWANA huuchunguza kila moyo na kujua kila kusudi la kila fikira. Ukimtafuta, ataonekana kwako, bali kama ukimwacha, yeye atakukataa wewe milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nawe Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa kujitoa kwa moyo wote na kwa nia ya kumkubali, kwa maana bwana huuchunguza kila moyo na kujua kila kusudi la kila fikira. Ukimtafuta, ataonekana kwako; bali kama ukimwacha, yeye atakukataa milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote na fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nawe Solomoni mwanangu, umjue Mungu wa baba yako, na umtumikie kwa moyo wako wote na kwa nia thabiti; yeye Mwenyezi-Mungu huchunguza mioyo na anafahamu mipango na fikira za binadamu. Ukimtafuta yeye, utamwona; lakini ukimwacha, atakutupilia mbali milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe mwanangu Salomo, mjue Mungu wa baba yako, umtumikie kwa moyo wote mzima na kwa roho ipendezwayo naye! Kwani Bwana huichungua mioyo yote na kuyatambua mawazo yote, iliyoyatunga. Utakapomtafuta, atakuonekea; lakini ukimwacha, atakutupa kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Nawe Solomono mwana wangu, umujue Mungu wa baba yako, na umutumikie kwa moyo wako wote na kwa nia nzuri; yeye Yawe anachunguza mioyo na anafahamu mipango na mafikiri ya mwanadamu. Ukimutafuta yeye, utamwona; lakini ukimwacha, atakutupilia mbali milele.