1 Chronicles 29:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ukuu ni wako, ee Mwenyezi-Mungu, una nguvu, utukufu, ushindi na enzi. Vyote vilivyoko mbinguni na duniani ni vyako. Ee Mwenyezi-Mungu, ufalme ni wako, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Mwenyezi Mungu, na utukufu na enzi na uzuri, kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani ni chako wewe. Ee Mwenyezi Mungu, ufalme ni wako; umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Bwana, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na kushinda, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee Bwana, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ukuu ni wako, ee Mwenyezi-Mungu, una nguvu, utukufu, ushindi na enzi. Vyote vilivyoko mbinguni na duniani ni vyako. Ee Mwenyezi-Mungu, ufalme ni wako, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ukuu na uweza, ni vyako, Ee BWANA, na utukufu na enzi na uzuri, kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani ni chako wewe. Ee BWANA, ufalme ni wako, umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ukuu na uweza, ni vyako, Ee bwana, na utukufu na enzi na uzuri, kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani ni chako wewe. Ee bwana, ufalme ni wako; umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee BWANA, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na ushindi, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee BWANA, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ukuu ni wako, ee Mwenyezi-Mungu, una nguvu, utukufu, ushindi na enzi. Vyote vilivyoko mbinguni na duniani ni vyako. Ee Mwenyezi-Mungu, ufalme ni wako, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe Bwana ndiwe mwenye ukuu na uwezo na utukufu na ung'avu na urembo, kwani yote yaliyomo mbinguni na nchini ni yako, Bwana, ndiwe mfalme wao na kichwa chao yote kwa kuwa huko juu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee BWANA, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na kushinda, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee BWANA, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ukubwa ni wako, ee Yawe, una nguvu, utukufu, ushindi na mamlaka. Vyote vinavyokuwa mbinguni na katika dunia ni vyako. Ee Yawe, ufalme ni wako, nawe umetukuzwa, uko mukubwa juu ya vitu vyote.