1 Chronicles 29:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, mfalme Daudi aliwaambia wote waliokusanyika, “Msifuni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.” Na wote waliokusanyika wakamtukuza Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao, wakamsujudia na kumwabudu Mwenyezi-Mungu na kumtolea mfalme Daudi heshima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Daudi akawaambia kusanyiko lote, “Mhimidini Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.” Hivyo wote wakamhimidi Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao. Wakasujudu, na nyuso zao zikagusa chini mbele za Mwenyezi Mungu na mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Daudi akawaambia kusanyiko lote, Haya, mhimidini Bwana, Mungu wenu. Basi kusanyiko lote wakamhimidi Bwana, Mungu wa baba zao, wakainama vichwa vyao, wakamsujudia Bwana, na mfalme naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, mfalme Daudi aliwaambia wote waliokusanyika, “Msifuni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.” Na wote waliokusanyika wakamtukuza Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao, wakamsujudia na kumwabudu Mwenyezi-Mungu na kumtolea mfalme Daudi heshima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote, “Mhimidini BWANA Mungu wenu.” Hivyo wote wakamhimidi BWANA, Mungu wa baba zao, wakasujudu na kuanguka kifudifudi mbele za BWANA na mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote, “Mhimidini bwana Mwenyezi Mungu wenu.” Hivyo wote wakamhimidi bwana, Mungu wa baba zao. Wakasujudu na kuanguka kifudifudi mbele za bwana na mfalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Daudi akawaambia kusanyiko lote, Haya, mhimidini BWANA, Mungu wenu. Basi kusanyiko lote wakamhimidi BWANA, Mungu wa baba zao, wakainamisha vichwa vyao, wakamsujudia BWANA, na mfalme naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, mfalme Daudi aliwaambia wote waliokusanyika, “Msifuni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.” Na wote waliokusanyika wakamtukuza Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao, wakamsujudia na kumwabudu Mwenyezi-Mungu na kumtolea mfalme Daudi heshima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akauambia huo mkutano wote: Mtukuzeni Bwana Mungu wenu! Ndipo, watu wote wa mkutano walipomtukuza Bwana Mungu wa baba zao na kujiinamisha na kumwangukia Bwana na mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Daudi akawaambia kusanyiko lote, Haya, mhimidini BWANA, Mungu wenu. Basi kusanyiko lote wakamhimidi BWANA, Mungu wa baba zao, wakainama vichwa vyao, wakamsujudia BWANA, na mfalme naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, mufalme Daudi akawaambia wote waliokusanyika: “Mumusifu Yawe, Mungu wenu.” Na wote waliokusanyika wakamutukuza Yawe, Mungu wa babu zao, wakainama mbele yake na kumwabudu Yawe na kumutolea mufalme Daudi heshima.