1 Chronicles 29:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakamtolea tambiko Mwenyezi-Mungu. Siku ya pili yake wakamtolea sadaka za kuteketezwa: Mafahali 1,000, wanakondoo 1,000, pamoja na sadaka zao za vinywaji na tambiko nyingi kwa ajili ya Waisraeli wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya pili yake, wakamtolea Mwenyezi Mungu dhabihu na sadaka za kuteketezwa: mafahali elfu moja, kondoo dume elfu moja, na wana-kondoo dume elfu moja, pamoja na sadaka za vinywaji, na sadaka nyingine nyingi sana kwa ajili ya Israeli yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamtolea Bwana dhabihu, wakamchinjia Bwana sadaka za kuteketezwa, siku ya pili yake, yaani, ng'ombe elfu, na kondoo waume elfu, na wana-kondoo elfu, pamoja na sadaka zao za vinywaji, na dhabihu nyingi kwa ajili ya Israeli wote;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakamtolea tambiko Mwenyezi-Mungu. Siku ya pili yake wakamtolea sadaka za kuteketezwa: mafahali 1,000, wanakondoo 1,000, pamoja na sadaka zao za vinywaji na tambiko nyingi kwa ajili ya Waisraeli wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya pili yake wakamtolea BWANA dhabihu na sadaka za kuteketezwa: mafahali 1,000, kondoo waume 1,000 na wana-kondoo waume 1,000, pamoja na sadaka za kinywaji na sadaka nyingine nyingi sana kwa ajili ya Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya pili yake wakamtolea bwana dhabihu na sadaka za kuteketezwa: mafahali 1,000, kondoo dume 1,000 na wana-kondoo dume 1,000, pamoja na sadaka za kinywaji na sadaka nyingine nyingi sana kwa ajili ya Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku ya pili yake, wakamtolea BWANA dhabihu, wakamchinjia BWANA sadaka ya kuteketezwa, yaani, ng'ombe elfu moja, na kondoo dume elfu moja, na wana-kondoo elfu moja, pamoja na sadaka zao za vinywaji, na dhabihu nyingi kwa ajili ya Israeli wote;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakamtolea tambiko Mwenyezi-Mungu. Siku ya pili yake wakamtolea sadaka za kuteketezwa: Mafahali 1,000, wanakondoo 1,000, pamoja na sadaka zao za vinywaji na tambiko nyingi kwa ajili ya Waisraeli wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamtolea Bwana ng'ombe za tambiko; kesho yake siku hiyo wakamteketezea Bwana madume ya ng'ombe elfu na madume ya kondoo elfu na wana kondoo elfu pamoja na kumtolea vinywaji vya tambiko na ng'ombe nyingi nyingine za tambiko kwa ajili ya Waisiraeli wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamtolea BWANA dhabihu, wakamchinjia BWANA sadaka za kuteketezwa, siku ya pili yake, yaani, ng’ombe elfu, na kondoo waume elfu, na wana-kondoo elfu, pamoja na sadaka zao za vinywaji, na dhabihu nyingi kwa ajili ya Israeli wote;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamutolea Yawe sadaka. Kesho yake wakamutolea sadaka za kuteketezwa kwa moto: ngombe dume elfu moja, wana-kondoo elfu moja, pamoja na sadaka zao za vinywaji na sadaka nyingi kwa ajili ya Waisraeli wote.