1 Chronicles 29:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi siku hiyo walikula na kunywa kwa furaha kuu mbele ya Mwenyezi-Mungu. Wakamtawaza Solomoni mwana wa Daudi, mara ya pili. Wakampaka mafuta awe mtawala kwa jina la Mwenyezi-Mungu, na Sadoki awe kuhani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakala na kunywa kwa furaha kubwa mbele za Mwenyezi Mungu siku ile. Wakamtawaza Sulemani mwana wa Daudi mara ya pili kuwa mfalme, wakampaka mafuta mbele za Mwenyezi Mungu ili awe mfalme na Sadoki kuwa kuhani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakala na kunywa mbele za Bwana siku ile, kwa furaha kuu. Wakamtawaza Sulemani, mwana wa Daudi, mara ya pili, wakamtia mafuta mbele za Bwana, awe mkuu, na Sadoki awe kuhani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi siku hiyo walikula na kunywa kwa furaha kuu mbele ya Mwenyezi-Mungu. Wakamtawaza Solomoni mwana wa Daudi, mara ya pili. Wakampaka mafuta awe mtawala kwa jina la Mwenyezi-Mungu, na Sadoki awe kuhani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakala na kunywa kwa furaha kubwa mbele za BWANA siku ile. Wakamtawaza Solomoni mwana wa Daudi mara ya pili kuwa mfalme, wakamtia mafuta kwa ajili ya BWANA ili awe mfalme na Sadoki kuwa kuhani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakala na kunywa kwa furaha kubwa mbele za bwana siku ile. Wakamtawaza Sulemani mwana wa Daudi mara ya pili kuwa mfalme, wakamtia mafuta kwa ajili ya bwana ili awe mfalme na Sadoki kuwa kuhani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakala na kunywa mbele za BWANA siku ile, kwa furaha kuu. Wakamtawaza Sulemani, mwana wa Daudi, mara ya pili, wakamtia mafuta mbele za BWANA, awe mkuu, na Sadoki awe kuhani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi siku hiyo walikula na kunywa kwa furaha kuu mbele ya Mwenyezi-Mungu. Wakamtawaza Solomoni mwana wa Daudi, mara ya pili. Wakampaka mafuta awe mtawala kwa jina la Mwenyezi-Mungu, na Sadoki awe kuhani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakala, wakanywa mbele ya Bwana siku hiyo na kufurahi sana. Kisha wakamchukua Salomo, mwana wa Dawidi, mara ya pili, awe mfalme wao, wakampaka mafuta, awe mkuu aliye mtu wa Bwana, naye Sadoki wakampaka mafuta, awe mtambikaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakala na kunywa mbele za BWANA siku ile, kwa furaha kuu. Wakamtawaza Sulemani, mwana wa Daudi, mara ya pili, wakamtia mafuta mbele za BWANA, awe mkuu, na Sadoki awe kuhani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi siku ile wakakula na kunywa kwa furaha kubwa mbele ya Yawe. Kwa mara ya pili wakamuweka Solomono mwana wa Daudi kuwa mufalme. Wakamupakaa mafuta apate kuwa mutawala katika jina la Yawe, na Zadoki akuwe kuhani.