1 Chronicles 29:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu akampa Solomoni sifa nzuri machoni pa Waisraeli wote, akampa fahari ya kifalme ipitayo fahari ya mfalme awaye yote aliyeitawala Israeli kabla yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akamtukuza sana Sulemani mbele ya Waisraeli wote na kumvika fahari ya kifalme ambayo hakuna mfalme yeyote wa Israeli kabla yake aliwahi kuwa nayo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Bwana akamtukuza Sulemani mno machoni pa Israeli wote, akampa fahari ya kifalme ya kumpita mfalme awaye yote aliyekuwa kabla yake katika Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu akampa Solomoni sifa nzuri machoni pa Waisraeli wote, akampa fahari ya kifalme ipitayo fahari ya mfalme awaye yote aliyeitawala Israeli kabla yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akamtukuza sana Solomoni mbele ya Israeli wote na kumvika fahari ya kifalme ambayo hakuna mfalme ye yote wa Israeli kabla yake aliwahi kuwa nayo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akamtukuza sana Sulemani mbele ya Israeli wote na kumvika fahari ya kifalme ambayo hakuna mfalme yeyote wa Israeli kabla yake aliwahi kuwa nayo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye BWANA akamtukuza Sulemani mno machoni pa Israeli wote, akampa fahari ya kifalme ya kumpita mfalme awaye yote aliyekuwa kabla yake katika Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu akampa Solomoni sifa nzuri machoni pa Waisraeli wote, akampa fahari ya kifalme ipitayo fahari ya mfalme awaye yote aliyeitawala Israeli kabla yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akampatia Salomo ukuu uliozidi machoni pao Waisiraeli wote, akampa hata urembo wa kifalme kuupita wote, walioupata wengine waliokuwa mbele yake wafalme wa Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye BWANA akamtukuza Sulemani mno machoni pa Israeli wote, akampa fahari ya kifalme ya kumpita mfalme awaye yote aliyekuwa kabla yake katika Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akamupa Solomono sifa nzuri mbele ya Waisraeli wote, akamupa utukufu wa kifalme unaopita utukufu wa mufalme yeyote aliyeitawala inchi ya Israeli mbele yake.