1 Chronicles 29:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Habari za mfalme Daudi toka mwanzo hadi mwisho, zimeandikwa katika kumbukumbu za Samueli mwonaji, katika kumbukumbu za nabii Nathani na katika kumbukumbu za Gadi mwonaji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhusu matukio ya utawala wa Mfalme Daudi, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kumbukumbu za mwonaji Samweli, na kumbukumbu za nabii Nathani na kumbukumbu za mwonaji Gadi,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Habari za mfalme Daudi toka mwanzo hadi mwisho, zimeandikwa katika kumbukumbu za Samueli mwonaji, katika kumbukumbu za nabii Nathani na katika kumbukumbu za Gadi mwonaji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhusu matukio ya utawala wa Mfalme Daudi, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kumbukumbu za mwonaji Samweli, na kumbukumbu za nabii Nathani na kumbukumbu za mwonaji Gadi,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhusu matukio ya utawala wa Mfalme Daudi, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kumbukumbu za mwonaji Samweli, na kumbukumbu za nabii Nathani na kumbukumbu za mwonaji Gadi,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo hadi mwisho, angalia, zimeandikwa katika kumbukumbu za Samweli, mwonaji, na katika kumbukumbu za Nathani, nabii, na katika kumbukumbu za Gadi, mwonaji;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Habari za mfalme Daudi toka mwanzo hadi mwisho, zimeandikwa katika kumbukumbu za Samueli mwonaji, katika kumbukumbu za nabii Nathani na katika kumbukumbu za Gadi mwonaji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo mambo ya mfalme Dawidi, ya kwanza na ya mwisho tunayaona, yameandikwa penye mambo ya mtazamaji Samweli na penye mambo ya mfumbuaji Natani na penye mambo ya mchunguzaji Gadi;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Habari za mufalme Daudi toka mwanzo mpaka mwisho juu ya mambo ya utawala wake, uwezo wake, na mambo yaliyomupata yeye, Waisraeli, na falme zote katika inchi zimeandikwa katika vitabu vya nabii Samweli, katika vitabu vya nabii Natani, vilevile katika vitabu vya nabii Gadi.