1 Chronicles 29:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo watu wakafurahi kwa sababu walitoa kwa hiari, maana kwa moyo wao wote walimtolea Mwenyezi-Mungu kwa hiari, naye mfalme Daudi alifurahi sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa Mwenyezi Mungu. Mfalme Daudi pia akafurahi sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo hao watu wakafurahi, kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe, kwa sababu kwa ukamilifu wa moyo, kwa hiari yao wenyewe, wamemtolea Bwana; mfalme Daudi naye akafurahi kwa furaha kuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo watu wakafurahi kwa sababu walitoa kwa hiari, maana kwa moyo wao wote walimtolea Mwenyezi-Mungu kwa hiari, naye mfalme Daudi alifurahi sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa BWANA. Mfalme Daudi pia akafurahi sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa bwana. Mfalme Daudi pia akafurahi sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo hao watu wakafurahi, kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe, kwa moyo wao wote, kwa hiari yao wenyewe, wamemtolea BWANA; mfalme Daudi naye akafurahi sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo watu wakafurahi kwa sababu walitoa kwa hiari, maana kwa moyo wao wote walimtolea Mwenyezi-Mungu kwa hiari, naye mfalme Daudi alifurahi sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wakavifurahia hivyo, walivyovitoa kwa kupenda wenyewe, kwani kila alimtolea Bwana kwa kupenda kwa moyo wote mzima, naye mfalme Dawidi alifurahi na kuona furaha kubwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo hao watu wakafurahi, kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe, kwa sababu kwa ukamilifu wa moyo, kwa hiari yao wenyewe, wamemtolea BWANA; mfalme Daudi naye akafurahi kwa furaha kuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu watu wakafurahi kwa sababu walitoa kwa mapenzi yao, maana kwa moyo wao wote walimutolea Yawe kwa mapenzi yao, naye mufalme Daudi akafurahi sana.