1 Chronicles 3:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hawa ndio wana wa mfalme Daudi waliozaliwa wakati alipokuwa huko Hebroni: Amnoni, mzaliwa wake wa kwanza; mama yake aliitwa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili, Mkarmeli;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa walikuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni: Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli; wa pili, Danieli ambaye mama yake aliitwa Abigaili wa Karmeli;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi hawa ndio wana wa Daudi, aliozaliwa huko Hebroni; Amnoni, mzaliwa wa kwanza, mwana wa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili, Danieli, wa Abigaili, Mkarmeli;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hawa ndio wana wa mfalme Daudi waliozaliwa wakati alipokuwa huko Hebroni: Amnoni, mzaliwa wake wa kwanza; mama yake aliitwa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili, Mkarmeli;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa ndio waliokuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni: Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli; wa pili, Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili wa Karmeli;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa ndio waliokuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni: Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli; wa pili, Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili wa Karmeli;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi hawa ndio wana wa Daudi, waliozaliwa huko Hebroni; Amnoni, mzaliwa wa kwanza, mwana wa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili, Danieli, wa Abigaili, Mkarmeli;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hawa ndio wana wa mfalme Daudi waliozaliwa wakati alipokuwa huko Hebroni: Amnoni, mzaliwa wake wa kwanza; mama yake aliitwa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili, Mkarmeli;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Dawidi, aliozaliwa Heburoni, walikuwa hawa: Wa kwanza Amunoni wa Mwizireeli Ahinoamu; wa pili Danieli wa Mkarmeli Abigaili;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi hawa ndio wana wa Daudi, aliozaliwa huko Hebroni; Amnoni, mzaliwa wa kwanza, mwana wa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili, Danieli, wa Abigaili, Mkarmeli;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hawa ndio wana wa mufalme Daudi waliozaliwa wakati alipokuwa kule Hebroni: Amunoni, muzaliwa wake wa kwanza. Mama yake aliitwa Ahinoamu, wa muji wa Yezereheli; wa pili: Danieli ambaye mama yake aliitwa Abigaili wa muji wa Karmeli; wa tatu: Abusaloma, ambaye mama yake aliitwa Maka, binti ya Talmai mufalme wa Gesuri; wa ine: Adonia, ambaye mama yake aliitwa Hagiti; wa tano: Sefatia, ambaye mama yake aliitwa Abitali; wa sita: Itiramu, ambaye mama yake aliitwa Egla.