1 Chronicles 3:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wafuatao ni wana wa mfalme Daudi alipokuwa Yerusalemu: Mkewe Bathshua, bintiye Amieli, alimzalia wana wanne: Himea, Shobabu, Nathani na Solomoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nao hawa ndio wana wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu: mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia wana wanne: Shamua, Shobabu, Nathani na Sulemani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hawa alizaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, wanne, wana wa Bathsheba, binti Eliamu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wafuatao ni wana wa mfalme Daudi alipokuwa Yerusalemu: mkewe Bathshua, bintiye Amieli, alimzalia wana wanne: Himea, Shobabu, Nathani na Solomoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nao hawa ndio watoto wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu: mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia Shamua, Shobabu, Nathani na Solomoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nao hawa ndio watoto wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu: mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia Shamua, Shobabu, Nathani na Sulemani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hawa alizaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, wanne, wana wa Bathsheba, binti Eliamu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wafuatao ni wana wa mfalme Daudi alipokuwa Yerusalemu: Mkewe Bathshua, bintiye Amieli, alimzalia wana wanne: Himea, Shobabu, Nathani na Solomoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo Yerusalemu alizaliwa hawa: Simea na Sobabu na Natani na Salomo; hawa wanne ni wa Bati-Sua, binti Amieli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hawa alizaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, wanne, wana wa Bathsheba, binti Eliamu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hawa ndio wana wa mufalme Daudi waliozaliwa alipokuwa Yerusalema: Muke wake Bati-Seba, binti ya Amieli, akamuzalia wana wane: Simea, Sobabu, Natani na Solomono.