1 Chronicles 4:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shimei alikuwa na wana kumi na sita na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na wana wengi, na jamii yake pia haikuongezeka kama kabila la Yuda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Shimei alikuwa na wana kumi na sita, na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na watoto wengi, hivyo ukoo wao wote haukuwa na watu wengi kama ukoo wa Yuda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Shimei alikuwa na wana wa kiume kumi na sita, na wana wa kike sita; walakini nduguze walikuwa hawana watoto wengi, tena jamaa yao yote haikuongezeka sana kwa mfano wa wana wa Yuda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shimei alikuwa na wana kumi na sita na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na wana wengi, na jamii yake pia haikuongezeka kama kabila la Yuda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Shimei alikuwa na wana kumi na sita, na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na watoto wengi, hivyo ukoo wao wote haukuwa na watu wengi kama ukoo wa Yuda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Shimei alikuwa na wana kumi na sita, na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na watoto wengi, hivyo ukoo wao wote haukuwa na watu wengi kama ukoo wa Yuda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Shimei alikuwa na wana wa kiume kumi na sita, na wana wa kike sita; lakini nduguze walikuwa hawana watoto wengi, tena jamaa yao yote haikuongezeka sana kama wana wa Yuda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shimei alikuwa na wana kumi na sita na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na wana wengi, na jamii yake pia haikuongezeka kama kabila la Yuda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Simei alikuwa mwenye wana wa kiume kumi na sita na wana wa kike sita, lakini ndugu zake hawakuwa na wana wengi, nao ukoo wao wote haukupata watu wengi kama wana wa Yuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Shimei alikuwa na wana wa kiume kumi na sita, na wana wa kike sita; walakini nduguze walikuwa hawana watoto wengi, tena jamaa yao yote haikuongezeka sana kwa mfano wa wana wa Yuda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Simei alikuwa na wana kumi na sita na wabinti sita, lakini wandugu zake hawakukuwa na wana wengi, na jamaa yake vilevile haikuongezeka kama kabila la Yuda. Miji walimokuwa wakiishi mpaka wakati wa utawala wa mufalme Daudi ilikuwa: Beri-Seba, Molada, Hasari-Suali, Biliha, Ezemi, Toladi, Betueli, Horma, Ziklagi, Beti-Makaboti, Hasari-Susimu, Beti-Biri na Sarayimu, Etamu, Aini, Rimoni, Tokeni na Asani, pamoja na vijiji kandokando ya miji hiyo mpaka Bali. Hayo ndiyo yaliyokuwa makao yao, nao wakaandika majina yao katika vitabu vya vizazi vyao.