1 Chronicles 4:40 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, walipata malisho tele, tena mazuri sana na pia nchi ilikuwa wazi, tulivu na yenye amani, kwani wenyeji wa nchi hiyo wa hapo awali walikuwa Wahamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huko walipata malisho mengi mazuri, nayo nchi ilikuwa na nafasi kubwa, yenye amani na utulivu. Baadhi ya Wahamu walikuwa wameishi huko awali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaona malisho ya unono, mazuri, na nchi yenyewe ilikuwa na nafasi, tena imetulia, na kuwa na amani; kwani waliokaa huko zamani walikuwa watu wa Hamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, walipata malisho tele, tena mazuri sana na pia nchi ilikuwa wazi, tulivu na yenye amani, kwani wenyeji wa nchi hiyo wa hapo awali walikuwa Wahamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huko walipata malisho mengi mazuri, nayo nchi ilikuwa na nafasi kubwa, yenye amani na utulivu. Baadhi ya Wahamu waliishi huko zamani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huko walipata malisho mengi mazuri, nayo nchi ilikuwa na nafasi kubwa, yenye amani na utulivu. Baadhi ya Wahamu waliishi huko zamani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaona malisho ya unono, mazuri, na nchi yenyewe ilikuwa wazi, tulivu na yenye amani; kwani waliokaa huko zamani walikuwa watu wa Hamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo, walipata malisho tele, tena mazuri sana na pia nchi ilikuwa wazi, tulivu na yenye amani, kwani wenyeji wa nchi hiyo wa hapo awali walikuwa Wahamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaona malisho mema ya kuwanonesha, nayo ile nchi ilikuwa pana pande zote, tena ilikuwa yenye utulivu na utengemano, kwani kale watu wa Hamu walikuwa wakikaa huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaona malisho ya unono, mazuri, na nchi yenyewe ilikuwa na nafasi, tena imetulia, na kuwa na amani; kwani waliokaa huko zamani walikuwa watu wa Hamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kule, walipata malisho tele, tena mazuri sana na tena inchi ilikuwa wazi, tulivu na yenye amani, maana wenyeji wa inchi hiyo wa zamani walikuwa wazao wa Hamu.